Bikini ni jina la atolli ya Mikronesia kwenye nchi ya Visiwa vya Marshall katika Pasifiki. Mahali pake ni 11°30'N 165°25'E. Ina visiwa vidogo 36 vinavyozungusha hori ya ndani yenye urefu wa kilomita 4o na eneo la km² 594,2.

Ramani ya atolli ya Bikini. Kisiwa kidogo cha Bikini chenyewe kipo pembe ya kaskazini-mashariki. "Able" na Baker" ni mahali pa milipuko miwili ya kwanza mwaka 1946.

Makaburi ya manowari

hariri

Mwisho wa vita kuu ya pili ya dunia jeshi la Marekani lilizamisha manowari zilizoharibika na kutohitajiwa tena kwenye hori ya ndani ya atolli.

Milipuko ya kinyuklia

hariri

Kati ya miaka 1946 na 1958 ilikuwa mahali pa majaribio ya kinyuklia ya Marekani. Zaidi ya mabomu 20 za kinyuklia zililipuliwa hapa. Wakazi waliondolewa kabla ya majaribio na atolli ikawa kituo cha kijeshi. Waliporudi baada ya mwisho wa milipuko, wengi waligonjeka kutokana na mnururisho unaoendelea. Ilikuwa lazima kuwaondoa tena na sasa wanakaa kwenye kisiwa cha Kili au wengine katika mtaa wa vibanda kwenye atolli ya Majuro.

Bikini kama vazi la kuogelea la wanawake

hariri

Bikini imekuwa pia jina la vazi la kuogelea kwa wanawake lenye vipande viwili lililoanzishwa siku chache baada ya mlipuko wa kwanza mwaka 1946. Mwuzaji wa mavazi hayo alitumia jina lililokuwa maarufu kama matangazo ya bure.

  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.