Binyavanga Wainaina

Binyavanga Wainaina (18 Januari 1971 - 21 Mei 2019) alikuwa mwandishi kutoka nchini Kenya.

Binyavanga Wainaina

MaishaEdit

Alizaliwa Nakuru, nchini Kenya. Alihudhuria masomo ya msingi na sekondari nchini Kenya kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Transkei, Afrika Kusini.

Baada ya kumaliza masomo yake alihamia katika jiji la Cape Town ambapo alifanya kazi kama mwandishi wa kujitegemea wa masuala ya chakula na utalii.

Mwezi Julai 2002 Binyavanga alishinda Tuzo ya Caine kwa Uandishi wa Kiafrika. Yeye ndiye mwanzilishi wa jarida la fasihi la Kwani?, ambalo linachukuliwa kuwa ndio gazeti kuu la masuala ya fasihi toka Afrika Mashariki.

Aliaandika riwaya yake ya kwanza iitwayo The Fallen World of Appearances. Mwaka 2003 alipata tuzo toka Chama cha Wachapishaji wa Kenya (Kenya Publishers Association) kutokana na juhudi zake za kuendeleza fasihi ya Kenya.

Alisomea shahada ya pili ya Uandishi wa Ubunifu katika Chuo Kikuu cha East Anglia. Kazi zake zimetoka katika magazeti na majarida mbalimbali kama vile National Geographic, The East African, The Sunday Times (ya Afrika Kusini), The Guardian (ya Uingereza).

Baadhi ya kazi alizoandika ni:

  • Discovering Home (Hadithi fupi, G21Net, 2001)
  • An Affair to Dismember (Hadithi fupi)
  • Beyond the River Yei: Life in the Land Where Sleeping is a Disease (Riwaya ya picha pamoja na Steven Torfinn, Kwani Trust).

Kupata UKIMWIEdit

Tarehe 1 Disemba 2016, katika siku ya UKIMWI Duniani, Wainaina alitangaza kupitia akaunti yake ya Twitter kwamba amethibitika kuwa na UKIMWI.[1]

KifoEdit

Wainaina amefariki dunia baada ya kupata ugonjwa majira ya saa nne usiku ya tarehe 21 Mei, 2019, katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi, hiyo ni kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wanandugu.[2]

MarejeoEdit

  1. Binyavanga Wainaina [@BinyavangaW] (1 December 2016). i am HiV Positive, and happy.
  2. Binyavanga Wainaina, 1971–2019, RIP (en-US).

Viungo vya njeEdit