Caterina Murino
Caterina Murino (amezaliwa 15 Septemba 1977) [1] ni mwigizaji wa Kiitaliano.
Caterina Murino |
---|
Maisha na Taaluma
haririAlizaliwa mjini Cagliari, Sardinia, nchini Italia. Yeye mwanzowe alitaka kuwa daktari, lakini alibadilisha kazi yake na kuingilia kazi ya upambe (beauty pageants) baada ya kutofaulu mtihani wa kiingilio wa kusomea udaktari.[2] Yeye alikuwa nambari ya tano katika mashindano ya Miss Italy mnamo 1996. [3] Mwaka 1999 na 2000, alisomea masomo ya maigizo katika "Cinema of Theatre of Francesca de Sapio", na alionekana katika utayarishaji wa Richard III na tamthiliya za lugha ya Kiitaliano. Ameanza kazi katika televisheni mwaka 2002. Yeye alipata umaarufu kote duniani baada kuigiza kama Solange mnamo [[2006 kwenye kipindi cha James Bond James Bond iitwayo Casino Royale.|2006 kwenye kipindi cha James Bond James Bond iitwayo Casino Royale. ]]
Yeye huzungumza Kiitalia, Kihispania, Kiingereza na Kifaransa. [4] Amekuwa anaoishi mjini Paris tangu mwaka wa 2004. Mwaka wake wa kuzaliwa unaripotiwa kuwa 1974 mara nyingine,[5] ingawa tovuti yake rasmi inatoa mwaka wa 1977.
Filamu alizoigiza
hariri- Nowhere (2001)
- Il Regalo Di Anita (2002)
- L'Enquête Corse (2004)
- L'Amour aux Trousses (2004)
- Elonora d'arborea (2005)
- Les Bronzes 3 (2005)
- Vientos de agua (2006)
- Casino Royale (2006)
- St Trinian's (2007)
- Il seme della discordia (2008)
- The Garden of Eden (2008)
- XIII (2009)
Marejeo
hariri- ↑ Gary Susman (2006-08-08). "Solange, It's Been Good to Know You". Entertainment Weekly. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-08-25. Iliwekwa mnamo 2008-03-22.
It's already been a rapid rise to stardom for the 28-year-old Murino...
- ↑ Rodney Chester (2006-12-08). "Why I love Caterina". The Courier-Mail. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-12-30. Iliwekwa mnamo 2008-03-22.
- ↑ John Preston (2006-12-11). "The Royale Ascent". Daily Telegraph. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-12-12. Iliwekwa mnamo 2008-03-22.
- ↑ Helen Barlow (2006-11-17). "Falling into bed with Bond". The Courier-Mail. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-06-02. Iliwekwa mnamo 2008-03-22.
- ↑ Kwa mfano, angalia Caterina Murino at the Internet Movie Database