Cherero
Ndege wadogo kiasi wa familia Psittaculidae
Cherero | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 9:
|
Cherero au kasuku-mapenzi ni ndege wa jenasi Agapornis katika familia Psittaculidae. Ndege hawa ni aina ya kasuku wadogo na wana rangi kali. Mkia wao ni mfupi kuliko kasuku wengine lakini kama hawa miguu yao ina vidole viwili vikabilivyo mbele na viwili vikabilivyo nyuma. Domo lao lina nguvu sana na mataya yamepindika kwa pande za kuelekea kama koleo. Cherero wanatokea Afrika na Madagaska. Hula matunda, mboga, mbegu na pengine wadudu. Dume na jike wanaishi pamoja kwa maisha yao yote. Hupitisha muda mrefu wakikaa karibu sana. Kwa hivyo huitwa kasuku-mapenzi pia. Jike huyataga mayai 3-8 tunduni kwa mti.
Spishi
hariri- Agapornis canus, Cherero Kichwa-kijivu Madagascar au Grey-headed Lovebird)
- Agapornis c. ablectaneus
- Agapornis c. canus
- Agapornis fischeri, Cherero Uso-machungwa (Fischer's Lovebird)
- Agapornis lilianae, Cherero wa Lilian (Lilian's au Nyasa Lovebird)
- Agapornis nigrigenis, Cherero Mashavu-meusi (Black-cheeked Lovebird)
- Agapornis personatus, Cherero Shingo-njano (Masked au Yellow-collared Lovebird)
- Agapornis pullarius, Cherero Uso-mwekundu (Red-faced au Red-headed Lovebird)
- Agapornis p. pullarius
- Agapornis p. ugandae
- Agapornis roseicollis, Cherero Uso-pinki (Peach-faced au Rosy-faced Lovebird)
- Agapornis r. catumbella
- Agapornis r. roseicollis
- Agapornis swindernianus, Cherero Mkufu-mweusi (Black-collared au Swindern's Lovebird)
- Agapornis s. emini
- Agapornis s. swindernianus
- Agapornis s. zenkeri
- Agapornis taranta, Cherero Habeshi (Abyssinian or Black-winged Lovebird)
Picha
hariri-
Cherero kichwa-kijivu
-
Cherero kichwa-machungwa
-
Cherero wa Lilian
-
Cherero mashavu-meusi
-
Cherero shingo-njano
-
Cherero uso-mwekundu
-
Cherero uso-pinki
-
Cherero mkufu-mweusi
-
Cherero Habeshi
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Cherero kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |