Chuo Kikuu cha Iringa (UoI)
Chuo kikuu cha Iringa ni chuo kikuu binafsi kinachopatikana mkoani Iringa, Tanzania.[1]
Historia
haririMwaka 1995 chuo kikuu cha Iringa kilianza, kikiwa kama chuo kikuu kishiriki chini ya chuo kikuu cha Tumaini[2].
Mwaka 1997 kikaanza kutoa astashahada, stashahada pamoja na shahada.
Tarehe 25 Oktoba 2013, chuo kikuu cha Iringa kikapewa rasmi hadhi ya chuo kikuu kutoka chuo kikuu kishiriki.
Taaluma
haririChuo kikuu cha Iringa kina vitivo sita, ambavyo ni:
- Kitivo cha Sheria
- Kitivo cha Teolojia
- Kitivo cha Saikolojia
- Kitivo cha Sayansi na Elimu
- Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii
- Kitivo cha Biashara na Uchumi
Vitivo hivyo vinavyotoa elimu katika fani mbalimbali kwa ngazi za:
- Astashahada
- Stashahada
- Shahada
- Shahada ya Uzamili
Marejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2021-06-24. Iliwekwa mnamo 2019-11-08.
- ↑ "Historia ya chuo kikuu Iringa". www.uoi.ac.tz (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2019-11-08.
Viungo vya nje
haririKigezo:Vyuo vikuu vya Tanzania
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Iringa (UoI) kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |