Chura wa Kihansi
Chura wa Kihansi (Nectophrynoides asperginis, Kihansi Spray Toad) ni chura mdogo aliye kienyeji katika eneo la Kihansi, Tanzania pekee.[3] [4] Spishi hiyo inazaa hai na inakula wadudu. [3] Mwaka 1999 mazingira asili yaliathiriwa na ujenzi wa Lambo la Kihansi. Chura wa Kihansi kwa sasa ameainishwa kama aliyetoweka porini lakini spishi hii inaendelea nje ya eneo lake la asili ikitunzwa katika hifadhi.
Chura wa Kihansi | |
---|---|
Kihansi spray toad at the Toledo Zoo | |
Hali ya hifadhi
| |
Uainishaji wa Kisayansi | |
Himaya: | Animalia |
Faila: | Chordata |
Class: | Amphibia |
Oda: | Anura |
Familia: | Bufonidae |
Jenasi: | Nectophrynoides |
Spishi: | N. asperginis
|
Jina la kibiolojia | |
Nectophrynoides asperginis Poynton, Howell, Clarke & Lovett, 1999
|
Makazi
haririKiasili chura huyu alipatikana pekee katika eneo dogo la hekta 2 (ekari 5) chini ya maporomoko ya maji ya Mto Kihansi katika mtelemko wa Udzungwa kwenye Mkoa wa Iringa nchini Tanzania. [5] Korongo la Kihansi lina urefu wa kilomita 4 likielekea kaskazini-kusini. [6]
Manyunyu ya maporomoko yaliunda mlia mwembamba mwenye mazingira ya pekee yaliyokuwa nyumbani wa chura huyu.[6] Ardhi nyevu hizi zilikuwa na uoto mnene wenye nyasi ikiwa ni pamoja na nyasi za Panicum, Selaginella kraussiana na kangaga (Tectaria gemmifera). [6] Maeneo ndani ya maeneo ya kunyunyizia maji ya maporomoko ya maji yalikuwa na halijoto isiyobadilika sana na unyevu wa 100%. [6]
Tangu kujengwa kwa lambo la Kihansi kwenye mwaka 1999 mfumo wa kunyunyizia uliwekwa kwa shabaha ya kutunza uhai wa chura unaolenga kuiga hali ya kiasili. Lakini mamlaka ulichelewa kuweka mfumo huu mapema[7] na chura zote za eneo hili walitoweka katika muda wa miaka michache.
Chura wengine wa spichi hiyo walitafutwa katika mazimgira ya maporomoko mengine ya maji kwenye miinuko ya Milima ya Udzungwa lakini hawakupatikana. [8]
Ufugaji wa chura
haririMpango wa ufugaji mbali na eneo la asili ulianzishwa mnamo mwaka 2001 kwa lengo la kuhifadhi spishi hiyo. Chura 500 walichukuliwa Kihansi na kupelekwa zoo sita.[9] [10] [11] Zoo mbili pekee za Bronx na Toledo ndizo zilizoweza kudumisha idadi ya chura. [10] Kwa sasa Toledo kuna vyura elfu kadhaa wa Kihansi, [9] [12] wengi wao wakiwa nje ya maonyesho. Zoo ya Bronx pia ina vyura elfu kadhaa wa Kihansi. [12]
Kurudishwa tena porini
haririTangu Agosti 2010 vyura kadhaa walirudishwa katika mazingira asili huko Kihansi kutoka Marekani[9] kwa kutumia kituo cha uenezi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. [11] [13] Kuna hatari kutokana na fungus fulani (chytrid fungus) inayoua vyura wengi[14].
Watafiti wanaona kwamba kuletwa tena kwa spishi hiyo porini kunaweza kuchukua muda kwa sababu inahitaji kuzoea mazingira ya porini ambayo inahitaji kutafuta chakula, kukwepa wanyama wanaowinda wanyama wengine, na kushinda magonjwa, tofauti na mazingira yaliyodhibitiwa ambayo waliishi wakati wa kufugwa Marekani. [15]
Tangu mwaka 2020 Shirika la Umeme Tanesco lilishiriki katika gharama za utunzaji wa vyura hao na kuwarudisha tena Tanzania kwa jumla ya TSh milioni 611.92[16]
Marejeo
hariri- ↑ IUCN SSC Amphibian Specialist Group (2015). "Nectophrynoides asperginis". IUCN Red List of Threatened Species. 2015: e.T54837A16935685. doi:10.2305/IUCN.UK.2015-2.RLTS.T54837A16935685.en. Retrieved 20 November 2021.
- ↑ "Appendices | CITES". cites.org.
- ↑ 3.0 3.1 Channing and Howell. (2006).
- ↑ Frost, Darrel R. (2015). "Nectophrynoides asperginis Poynton, Howell, Clarke, and Lovett, 1999". Amphibian Species of the World: an Online Reference. Version 6.0. American Museum of Natural History. Iliwekwa mnamo 9 Juni 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Menegon, M.; S. Salvidio; S.P. Loader (2004). "Five new species of Nectophrynoides Noble 1926 (Amphibia Anura Bufanidae) from the Eastern Arc Mountains, Tanzania". Tropical Zoology. 17: 97–121. doi:10.1080/03946975.2004.10531201.
{{cite journal}}
:|hdl-access=
requires|hdl=
(help) - ↑ 6.0 6.1 6.2 6.3 Channing, A.; Finlow-Bates, S.; Haarklau S.E.; Hawkes P.G. (2006). "The biology and recent history of the critically endangered Kihansi Spray Toad Nectophrynoides asperginis in Tanzania". Journal of East African Natural History. 95 (2): 117–138. doi:10.2982/0012-8317(2006)95[117:tbarho]2.0.co;2.
- ↑ IUCN SSC Amphibian Specialist Group (2015). "Nectophrynoides asperginis". IUCN Red List of Threatened Species. 2015: e.T54837A16935685. doi:10.2305/IUCN.UK.2015-2.RLTS.T54837A16935685.en. Retrieved 20 November 2021.
- ↑ Hitilafu ya kutaja: Invalid
<ref>
tag; no text was provided for refs named:0
- ↑ 9.0 9.1 9.2 "TZ to Tanzania: A Kihansi Spray Toad Fact Sheet". Toledo Zoo. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Novemba 2012. Iliwekwa mnamo 8 Januari 2011.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) Hitilafu ya kutaja: Invalid<ref>
tag; name "Toledo" defined multiple times with different content - ↑ 10.0 10.1 New York Times (1 February 2010).
- ↑ 11.0 11.1 Science Daily (17 August 2010).
- ↑ 12.0 12.1 ISIS (2012).
- ↑ Rhett A. Butler (4 Septemba 2008). "Yellow toad births offer hope for extinct-in-the-wild species". mongabay.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Julai 2012. Iliwekwa mnamo 9 Juni 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ https://www.tandfonline.com/doi/abs/10.1080/21564574.2020.1752313 Alan Channing, Gerald Misinzo, Andrew A Cunningham: Disease driven extinction in the wild of the Kihansi spray toad, Nectophrynoides asperginis, African Journal of Herpetology, Volume 69, 2020 - Issue 2 , https://doi.org/10.1080/21564574.2020.1752313
- ↑ Nahonyo, Cuthbert; Goboro, Ezekiel; Ngalason, Wilirk; Mutagwaba, Severinus; Ugomba, Richard; Nassoro, Mohammed; Nkombe, Emmanuel (2017-01-01). "Conservation efforts of Kihansi spray toad Nectophrynoides asperginis: its discovery, captive breeding, extinction in the wild and re-introduction". Tanzania Journal of Science (kwa Kiingereza). 43 (1): 23–35. ISSN 2507-7961.
- ↑ https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/siri-vyura-wa-kihansi-kutunzwa-marekani--4195398 Siri vyura wa Kihansi kutunzwa Marekani, Mwananchi tarehe11 April 2023
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chura wa Kihansi kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |