Dadra na Nagar Haveli

Dadra na Nagar Haveli ni eneo la muungano la jamhuri ya India. Dadra iko ndani ya jimbo la Gujarat, wakati Nagar Haveli iko kati ya jimbo hilo na lile la Maharashtra.

Mto Daman Ganga
Mahali pa Dadra na Nagar Haveli nchini India na ramani yake.

Eneo lote ni la kilometa mraba 487.

Ilikuwa koloni la Ureno hadi mwaka 1954, halafu ikamezwa na India mwaka 1961.

Makao makuu ni Silvassa.

Wakazi ni 342,853 (2011). Wengi wao (62%) ni wa makabila asili: Wavarli, Wadhodia, Wakokna n.k.

Upande wa dini, wanaongoza Wahindu (93.93%), halafu kuna Waislamu (3.75%), Wakristo (1.48%) n.k.