Daraja la Selander

Daraja la Selander ni daraja kwenye Barabara ya Ali Hassan Mwinyi (Bagamoyo Road) ambalo linavuka mto Msimbazi jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Daraja la Selander
English: Selander Bridge
YabebaBarabara ya Ali Hassan Mwinyi (leni 4)
YavukaMkondo wa Msimbazi (Msimbazi Creek)
MahaliOyster Bay, Dar es Salaam
MmilikiSerikali ya Tanzania
Urefumita 85
Kilifunguliwa1929
Anwani ya kijiografia6°47′46.69″S 39°16′52.81″E / 6.7963028°S 39.2813361°E / -6.7963028; 39.2813361
Daraja la Selander is located in Tanzania
Daraja la Selander
Mahali ya daraja nchini Tanzania

Daraja hili lilitengenezwa mwaka 1929 likapewa jina kwa kumbukumbu ya John Einar Selander aliyekuwa mkurugenzi wa kwanza wa ujenzi katika eneo la Tanganyika chini ya utawala wa Waingereza.[1]

Daraja hili lilipanuliwa na Japan International Cooperation Agency mnamo 1980[2] kuwa na njia 4 za magari.

Tangu mwaka 2019 daraja la pili limeanza kujengwa takriban mita 300 kando yake upande wa Oyster Bay.

Marejeo

hariri
  1. Brennan, James R.; Burton, Andrew; Lawi, Yusuf (2007). Dar es Salaam: Histories from an Emerging African Metropolis. Page 104, Mkuki na Nyota. Iliwekwa mnamo 7 Machi 2013.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "30 Years Of JICA Tanzania Office (1980-2010)" (PDF). Page 6, Japan International Cooperation Agency. 2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 7 Machi 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)