Chamayai
(Elekezwa kutoka Dasypeltis)
Chamayai | ||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Chamayai mabaka (Dasypeltis scabra)
| ||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||||
Spishi 13:
|
Chamayai ni spishi za nyoka wasio na sumu wa jenasi Dasypeltis katika familia Colubridae. Spishi zote zinapatikana katika Afrika.
Nyoka hawa sio warefu sana, kwa wastani sm 50-80 lakini kadhaa wanaweza kufika m 1.15. Rangi yao ni nyeusi, kijivu, kahawia au nyekundu na wana madoa au mabaka mara nyingi.
Chamayai hula mayai tu. Kwa hivyo wanatokea katika maeneo yenye miti mingi ambayo juu yao ndege wajenga matago yao. Wana vetebra kadhaa katika shingo zinazichomoza ndani ya koromeo. Baadha ya kumeza yai zima nyoka abinya koo lake na kutoboa yai kwa vetebra zile. Kisha akama uowevu wa yai na kutapika vipande vya ganda.
Spishi
hariri- Dasypeltis abyssina Chamayai Habeshi (Ethiopian egg-eating snake)
- Dasypeltis atra Chamayai-milima (Montane egg-eating snake)
- Dasypeltis bazi Chamayai wa Misri (Egyptian egg-eating snake)
- Dasypeltis confusa Chamayai Jakamoyo (Confusing egg-eating snake)
- Dasypeltis fasciata Chamayai wa Kati (Central African egg-eating snake)
- Dasypeltis gansi Chamayai Magharibi (West African egg-eating snake)
- Dasypeltis inornata Chamayai Kahawia (Southern brown egg eater)
- Dasypeltis latericia Chamayai Madoa-kahawia (Brown-spotted egg eater)
- Dasypeltis medici Chamayai Mashariki au Mwekundu (East African egg eater)
- Dasypeltis m. lamuensis Chamayai Mwekundu (Rufous egg eater)
- Dasypeltis m. medici Chamayai Mashariki (East African egg eater)
- Dasypeltis phillipsii Chamayai Mwekundu (Rufous egg eater)
- Dasypeltis palmarum Chamayai Miwaa (Palm egg eater)
- Dasypeltis parascabra Chamayai wa Ghuba ya Gini (Guinea Gulf egg eater)
- Dasypeltis sahelensis Chamayai wa Saheli (Sahel egg-eating snake)
- Dasypeltis scabra Chamayai Mabaka (Common egg-eating snake)
- Dasypeltis s. loveridgei Chamayai wa Loveridge
- Dasypeltis s. scabra Chamayai wa Kawaida
Picha
hariri-
Chamayai-milima
-
Chamayai-milima akimeza yai
-
Chamayai mashariki
-
Chamayai mabaka aliyemeza yai
Marejeo
hariri- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chamayai kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |