Debora
Debora (kwa Kiebrania דְּבוֹרָה|Dvora|Dəḇôrā, yaani Nyuki), mke wa Lapidothi, alikuwa nabii na mwamuzi wa taifa la Israeli katika karne ya 12 KK.
Mwanamke jasiri, aliweza kufanya mambo mengi makubwa katika historia ya wokovu kama inavyoelezwa na Biblia katika kitabu cha Waamuzi, sura 4-5.
Kwa miaka 40 hivi (kama 1160 KK-1121 KK) aliamua Waisraeli chini ya mtende kati ya Rama na Beteli.
Aliongoza pia jeshi la makabila kadhaa ya Israeli ya Kaskazini dhidi ya Yabin, mfalme mmojawapo wa Kanaani, mwenye makao makuu huko Hazor.
Wimbo wa Debora, unaoshangilia ushindi wake katika sura ya 5, ni shairi linalohesabiwa kati ya maandishi ya zamani zaidi ya Kiebrania, ukikadiriwa kuwa uliandikwa katika karne ya 12 KK.[1]
Tanbihi
hariri- ↑ Coogan, Michael D. (2011), The Old Testament, A Historical and Literary Introduction to the Hebrew Scriptures, Oxford University Press, ku. 214, 219
Marejeo
hariri- Bird, Phyllis (1974). "Images of Women in the Old Testament". Katika Rosemary Radford Ruether (mhr.). Religion and Sexism: Images of Women in the Jewish and Christian Traditions. Simon & Schuster. ISBN 0-671-21692-9.
- Brown, Cheryl Anne (1992). No Longer be Silent: First Century Jewish Portraits of Biblical Women: Studies in Pseudo-Philo's Biblical Antiquities and Josephus's Jewish Antiquities. Louisville, Ky.: Westminster J. Knox Press. ISBN 0-664-25294-X.
- Deen, Edith (1955). All the Women of the Bible. New York: Harper & Row.
- Lacks, Roslyn (1979). Women and Judaism: Myth, History, and Struggle. Garden City, N.Y.: Doubleday. ISBN 0-385-02313-8.
- Otwell, John H. (1977). And Sarah Laughed: the Status of Woman in the Old Testament. Philadelphia: Westminster Press. ISBN 0-664-24126-3.
- Phipps, William E. (1992). Assertive Biblical Women. Westport, CT: Greenwood Press. ISBN 0-313-28498-9.
- Schroeder, Joy A. (2014). Deborah's Daughters: Gender Politics and Biblical Interpretation. New York: Oxford University Press. ISBN 978-0-19-999104-4.
- Williams, James G. (1982). Women Recounted: Narrative Thinking and the God of Israel. Sheffield: Almond Press. ISBN 0-907459-18-8.
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Viungo vya nje
hariri- Book of Judges article, Jewish Encyclopedia
- Debbora, Catholic Encyclopedia
- Biblical Hebrew Poetry - Reconstructing the Original Oral, Aural and Visual Experience
- Song of Deborah (Judges 5) Reconstructed
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Debora kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |