Diodori na Rodopiani

Diodori na Rodopiani (walifariki Afrodisia, Karia, leo nchini Uturuki) walikuwa Wakristo wa Dola la Roma waliopata kuwa wafiadini kwa kupigwa mawe hadi kufa na wananchi wenzao wakati wa dhuluma ya kaisari Dioklesyano[1].

Inasemekana Diodori alikuwa padri na Rodopiani shemasi[2].

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 30 Aprili[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.