Kiazi kikuu
(Elekezwa kutoka Dioscorea)
Kiazi kikuu (Dioscorea spp.) | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mmea wa kiazi kikuu
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Viazi vikuu au mitubwi (Kiing.: yam) ni mimea ya chakula iliyoainishwa katika familia Dioscoreaceae. Chakula ni sehemu nene za mizizi yake (kiazi) yenye wanga. Kiazi kikuu ni kubwa sana kuliko kiazi cha kizungu na hata kiazi kitamu. Mimea yake inapanda juu ya mimea au miti ingine na hupandwa mahali pengi pa Afrika, Asia, Amerika ya Kusini, Visiwa vya Karibi na Visiwa vya Pasifiki.
Spishi
hariri- Dioscorea alata, Mdanga au Mtubwi-zambarau (Purple yam)
- Dioscorea bulbifera, Kiazi kikuu kizaacho viazi juu (Air potato)
- Dioscorea cayennensis, Mtubwi au Kiazi kikuu njano (Yellow yam)
- Dioscorea dumetorum, Mkikwa au Kiazi kikuu kichungu (Bitter yam)
- Dioscorea esculenta, Kiazi kikuu kidogo (Lesser yam)
- Dioscorea hirtiflora, Mtipu au Kiazi kikuu msitu (Wild yam)
- Dioscorea opposita, Kiazi kikuu cha Uchina (Chinese yam)
- Dioscorea rotundata, Mtubwi au Kiazi kikuu cheupe (White yam)
- Dioscorea trifida, Kiazi kikuu cha Guyana (Cush-cush yam)
Picha
hariri-
Mdanga
-
Danga
-
Kiazi kikuu kizaacho viazi juu
-
Kiazi kilichokatika
-
Kiazi kikuu kidogo
-
Kiazi
-
Kiazi kikuu cha Uchina
-
Kiazi
-
Mtipu
-
Kiazi kikuu cha Guyana