Dizeli ni fueli inayofaa kuendesha injini ya dizeli. Kwa kawaida inapatikana kwa njia ya mwevusho wa mafuta ya petroli lakini kuna pia fueli zenye tabia za dizeli zinazotengenezwa kwa kutumia mafuta kutokana na biomasi ya mimea au mbegu za mimea na hii ni aina ya biofueli.

Tenki la gari linalobeba mafuta ya dizeli.

Jina la dizeli ni kumbukumbu ya mhandisi Mjerumani Rudolf Diesel aliyebuni injini maalumu.

Dizeli ya kawaida hutengenezwa kwa njia ileile kama petroli kutokana na mafuta ya petroli kwa njia ya mvevusho; ila tu diseli ni sehemu ile inayotoka baada ya petroli kama halijoto ya mafuta yanayochemshwa inazidi sentigredi 200. Mafuta hupashwa moto hadi dutu mbalimbali ndani yake hufikia kiwango cha kuchemka na kuwa gesi. Petroli ni nyepesi na kutangulia, halafu zinafuata mafuta ya taa na dizeli.

Kwa ajili ya matumizi ya injini mbalimbali matokeo ya mwevusho yanachanganywa na kukorogwa kwa shabaha ya kupata dizeli sanifu; mafuta asilia hutofautiana kikemia, kwa hiyo viwango vya viowevu vyepesi na vizitoa vinavyopatikana katika mwevusho vinatofautiana kila mara.

Injini za dizeli ni kubwa na nzito kuliko injini za petroli, kwa hiyo zinatumiwa zaidi kwa malori, mabasi na meli. Hii ni sababu ya kwamba katika nchi nyingi dizeli huuzwa kwa bei nafuu: kwa kuwa serikali inataka kupunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa zinazobebwa na malori hasa.

Lakini katika nchi kadhaa kuna pia motokaa ndogo ya abiria yenye injini za dizeli; hata kama bei ya injini ya dizeli inapaswa kuwa kubwa kiasi kuliko injini ya petroli, ile bei nafuu ya fueli hii inasababisha watu wengi kutafuta magari yenye injini ya dizeli.

Tanbihi hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dizeli kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.