Chozi (ndege)

(Elekezwa kutoka Dreptes)
Chozi
Chozi tumbo-njano
Chozi tumbo-njano
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Passeroidea
Familia: Nectariniidae (Ndege walio na mnasaba na chozi)
Vigors, 1825
Ngazi za chini

Jenasi 16:

Chozi ni ndege wadogo wa familia Nectariniidae. Spishi za jenasi kadhaa zinaitwa neli. Spishi nyingi sana zina rangi kali zinazong'aa juani kama metali. Manyoya ya kati ya mkia ni marefu sana katika spishi nyingine. Domo lao limepindika na hutumika kwa kutoa mbochi katika maua au wadudu katika matundu. Hula mbochi hasa na pengine maji ya matunda na wadudu pia. Wawindaji-buibui, ambao wamo pia katika familia hii, hula wadudu zaidi kuliko chozi.

Ndege hawa wanatokea kanda za tropiki na nusutropiki za Afrika, Asia na kaskazini mwa Australia. Tundu lao lina umbo la mfuko na limening'izika kwa vitawi vyembamba. Jike hutaga mayai 2-4.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri