Elizabeth Michael (maarufu kama Lulu; amezaliwa 16 Aprili 1995) ni mwigizaji wa filamu kutoka Tanzania. Mwaka wa 2013 alishinda tuzo ya Zanzibar International Film Festival kama msanii bora wa kike kupitia filamu "Foolish Age". Mwaka 2017 alitajwa na Tuzo za Vijana Afrika zifanyikazo nchini Ghana miongoni mwa vijana 100 wa Afrika wenye ushawishi mkubwa.

Elizabeth Michael
Faili:Elizabeth Michael2016.jpg
Elizabeth Michael (Lulu) katika 2016 Africa Magic Viewers Choice Awards Lagos,Nigeria
AmezaliwaDiana Elizabeth Michael Kimemeta
16/4/1995
Majina mengineLulu
MhitimuChuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania
Kazi yakeMwigizaji, mtayarishaji wa filamu,
Miaka ya kazi2000-hadi sasa

Maisha ya awali=

hariri

Elizabeth alizaliwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar Es Salaam Tanzania. Ni mtoto wa Lucrecia Kalugira na Michael Kimemeta.

Baadaye alijiunga na katika shule ya Remnant Academy ambapo alimaliza elimu ya msingi. Alipata kusoma Perfect Vision High School, St Mary's High School kwa ajili ya elimu ya sekondari. Baadaye alijiunga katika Chuo Cha Utumishi Wa Umma Tanzania (TPSC) akisomea kozi ya stashahada ya Rasilimali watu na Utawala (Diploma In Human Resources Management).

Uigizaji

hariri

Alianza kuigiza akiwa na umri wa miaka mitano mnamo mwaka 2000. Baadae alijiunga na kikundi cha Sanaa Kaole Group ambapo alikuwa pamoja na Steven Kanumba, Vincent Kigosi, Mwanaidi Suka na wengine wengi ambapo aliigiza tamthilia nyingi za runinga kama vile Gharika, Taswira, Zizimo na nyingine nyingi ambapo alikuwa akitumia jina la Lulu ambalo limekuwa maarufu mpaka leo.

Baadae alianza kuigiza filamu akiwa bado na Umri mdogo,a mbapo filamu yake ya kwanza ilikuwa Misukosuko akishirikiana na Jimmy Mponda. Mnamo mwaka 2006 aliigiza filamu iitwayo wema iliyoandaliwa na Game 1st Quality na badae filamu nyingine nyingi kama Family Tears,Ripple Of Tears,Passion,Dangerous Girl na nyingine nyingi.Mpaka sasa amepata kuigiza filamu zaidi ya thelathini

Pia amepata kufanya Igizo la redioni lililoitwa Wahapahapa Akitumia jina la Mainda. lililoandaliwa na Media For Development International wakishirikiana na Ubalozi wa Marekani,Wizara Ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na chuo cha Johns Hopkins University Center For Communication Programs cha Marekani Igizo hilo liliongozwa na mmarekani afanyaye shughuli zake Afrika Bwana Jordan Riber.

Pia Katika mradi huohuo wa Wahapahapa alipata kuigiza katika Video mbili za wasanii Lady Jay Dee iitwayo Shamba na Ya Enika iitwayo Changanya .Mradi wa Wahapahapa ulikuwa na lengo la kuelimisha jamii juu Ya malezi bora Ya mtoto katika kipindi cha ukuaji.

Mnamo August 2013 Lulu alizindua filamu Yake Iitwayo Foolish Age ambayo Ni filamu Yake ya kwanza kuitaarisha mwenyewe.Ilizinduliwa katika ukumbi wa Mlimani City uliopo Dar Es Salaam Na kuhudhuriwa Na mamia ya Watu.Foolish Age ilifanya vizuri sokoni Na ilipata kuonyeshwa katika Tamasha Kubwa La Kimataifa La Filamu Zanzibar (Zanzibar International Film Festival) ,na baadae kuteuliwa kuwania Filamu Inayopendwa na Lulu alishinda Muigizaji wa Filamu Wa Kike Anaependwa kupitia filamu hio katika Tuzo za Watu 2014.

Mnamo Mwaka 2015 Alizindua Filamu Yake ya pili Kama mtayarishaji iitwayo Mapenzi Ya Mungu .Filamu Hio ilionyeshwa katika Tamasha La Filamu La Kimataifa La Zanzibar (ZIFF) na mwaka 2016 ilishinda Filamu Bora Afrika Mashariki katika Tuzo Za Africa Magic Viewers Choice Awards zilizofanyika Lagos Nigeria.

Utangazaji

hariri

Amewahi Kuwa mtangazaji wa kipindi cha runinga kiitwacho watoto wetu Kinachorushwa na Runinga Ya ITV Tanzania Akiwa na umri mdogo mnamo mwaka 2004-2007

Pia mnamo mwaka 2014 na 2015 alikuwa mtangazaji wa mashindano Ya kutafuta vipaji vya uigizaji Tanzania yaitwayo Tanzania Movie Talents

Ubalozi na Matangazo

hariri
  • 2013/14 alichaguliwa Kuwa balozi wa tamasha la filamu liitwalo Dar Film Festival lililofanyika Dar es Salaam.
  • 2015 alifanya kazi na kampuni ya simu ya Airtel Tanzania kama mtangazaji wa kipindi cha Airtel Yatosha Tv Show.
  • Pia ni balozi wa kampuni ya Paisha Tanzania, ijushughulishayo na ufanyaji wa biashara mitandaoni
  • Pia aliteuliwa na kampuni ya Hengan Baby Products and Sanitary co ltd Kuwa balozi wa freestyle napkins bidhaa za wanawake kwa miaka miwili
  • Pia ni balozi wa Sinema Zetu International Film Festival tamasha la filamu linaloandaliwa Na chaneli ya Sinema Zetu ya kampuni ya Azam
  • Pia ni balozi wa Azania inajulikana kama pishi la Lulu, ni manager wa upcoming actor ajulikanae kama Suhelyht khan ambae jina lake halisi ni Suhely Tarmohammed.

Filamugrafia

hariri

Tamthilia

hariri
Mwaka Jina Uhusika Maelezo
2000's Zizimo Lulu Ilionyeshwa Na Independent Television Tanzania (ITV Tanzania)
Dira
Taswira
Baragumu
Gharika
Sayari
Tufani
Tetemo
Jahazi
Demokrasia Ilionyeshwa na Shirika la Utangazaji Tanzania/ Tanzania Broadcasting Corporation (TBC)
2017 Sarafu Jackline Sanga "Jack" Inaonyeshwa na Maisha Magic Bongo (Dstv)

Igizo la radio

hariri
Mwaka Jina Uhusika Maelezo
2009 Wahapahapa Mainda Ilirushwa na Radio One Tanzania

Filamu

hariri
Mwaka Filamu Uhusika Maelezo/Wahusika
2005 Misukosuko Part 2 Catherine Jimmy Mponda,Seba and Salama Salmin(Sandrah)
2006 Wema[1] Betty Akishirikiana na Senga
2007 Silent Killer Akishirikiana na Mohamed Nurdin(Chekibudi),Shumileta
2008 Family Tears[2] Lindah Akiwa na Steven Kanumba,Wema Sepetu,Jacqueline Wolper and Richard Bezendhout
Mtoto wa Nyoka
Lost Twins[3] Anitha Mdogo Akiwa na Steven Kanumba,Hashimu Kambi ,Suzan Lewis.
2009 Taste of Love [4] Akiwa na Aunty Ezekiel ,Blandina Chagula,Mahsein Awadh.
Ripple of Tears[5] Lizy Akiwa na Steven Kanumba
Passion Akiwa Jacqueline Wolper,Irene Uwoya,Yusuph Mlela,Hashim Kambi
Unfortunate Love[6] Akiwa na Steven Kanumba,Lisa Jensen,Zamda
Too Late Akiwa na Mahsein Awadh(Dr Cheni),Tumaini Bigirimana(Fifi),Issa Mussa
Reason To Die Nyina Akiwa na Mahsein Awadh (Dr Cheni)
2010 Family Disaster[7] Julieth Akiwa na Vincent Kigosi,Diana Kimaro
Crazy Love[8] Mwanafunzi Akiwa na Steven Kanumba,Shamsa Ford,Hemed Suleiman
My dreams[9] Akiwa Vincent Kigosi,Irene Uwoya,Shamsa Ford,Mahsein Awadh
2011 Birthday Party Akiwa na Salma Jabu(Nisha)
Ritazo[10] Akiwa na Riyama Ally Na Baraka
Tattoo
Confusion[11] Besta Akiwa na Diana Kimario,Hemedi Suleiman
2012 House Boy[12] Lulu Akiwa na Wema Sepetu,Kajala Masanja,and Mr Blue
Woman Of Principles[13] Linah Akiwa na Vincent Kigosi and Nargis Mohamed
Dangerous Girl[14] Hidaya
Mtoto wa Mbwa[15] Nice Akiwa na Simon Mwakapagata (Rado)
Yatima Asiyestahili[16] Njwele Akiwa Nice Mohamed(Mtunisy) and Jeniffer Kyaka
Oxygen[17] Akiwa na Sydney, Hashim Kambi,Grace Mapunda
2013 Foolish Age [18] Loveness Akiwa na Diana Kimaro and Hashimu Kambi
2014 Family Curse[19] Akiwa na Hashimu Kambi,Yusuph Mlela,Cathy Rupia
2015 Mapenzi Ya Mungu [20] Shikana Akiwa na Flora Mtegoa,Linah Sanga
2016 Ni Noma [21] Angela Akiwa na Kulwa Kikumba and Isarito Mwakalikamo

Kama mtayarishaji

hariri
  • Foolish Age
  • Mapenzi Ya Mungu
  • Ni Noma

Tuzo Alizoshinda

hariri
  • 2013 Zanzibar International Film Festival- Mwigizaji Bora wa Kike
  • 2014 Tuzo za watu - Mwigizaji wa Kike Anayependwa
  • 2016 Africa Magic Viewers Choice Awards- Filamu Bora Afrika Mashariki (Mapenzi Ya Mungu)
  • 2016 Swahili Fashion Week Awards - Style Icon Of The Year

Marejeo

hariri
  1. "Wema". www.bongocinema.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-18. Iliwekwa mnamo 2016-08-13.
  2. "Family Tears". www.bongocinema.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-09-16. Iliwekwa mnamo 2016-08-13.
  3. "The Lost Twins". www.bongocinema.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-18. Iliwekwa mnamo 2016-08-13.
  4. "Taste of Love". www.bongocinema.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-18. Iliwekwa mnamo 2016-08-13.
  5. "Ripple of Tears". www.bongocinema.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-17. Iliwekwa mnamo 2016-08-13.
  6. "Unfortunate Love". www.bongocinema.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-17. Iliwekwa mnamo 2016-08-13.
  7. "Family Disaster". www.bongocinema.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-18. Iliwekwa mnamo 2016-08-13.
  8. "Crazy Love". www.bongocinema.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-18. Iliwekwa mnamo 2016-08-13.
  9. "My Dreams". www.bongocinema.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-10-11. Iliwekwa mnamo 2016-08-13.
  10. "Ritazo". www.bongocinema.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-17. Iliwekwa mnamo 2016-08-13.
  11. "Confusion". www.bongocinema.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-18. Iliwekwa mnamo 2016-08-13.
  12. "House Boy". www.bongocinema.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-09-16. Iliwekwa mnamo 2016-08-13.
  13. "Woman of Principles". www.bongocinema.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-18. Iliwekwa mnamo 2016-08-13.
  14. "Dangerous Girl". www.bongocinema.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-10-06. Iliwekwa mnamo 2016-08-13.
  15. "Mtoto wa Mbwa". www.bongocinema.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-18. Iliwekwa mnamo 2016-08-13.
  16. "Yatima". www.bongocinema.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-18. Iliwekwa mnamo 2016-08-13.
  17. "Oxygen". www.bongocinema.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-18. Iliwekwa mnamo 2016-08-13.
  18. "Foolish Age". www.bongocinema.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-02-22. Iliwekwa mnamo 2016-08-13.
  19. "Family Curse". www.bongocinema.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-05-15. Iliwekwa mnamo 2016-08-13.
  20. Mwangoka, Nicky (20 Oktoba 2014). "Karibu Nyumbani: Mapenzi Ya Mungu: Filamu Ya Lulu Na Mama Kanumba".{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  21. "Tanzania: Elizabeth Michael 'Lulu' Set To Drop New Film Tomorrow". celebafrica.com. 16 Septemba 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Septemba 2016. Iliwekwa mnamo 18 Julai 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Elizabeth Michael kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.