Erakla wa Aleksandria

Erakla wa Aleksandria (alifariki Aleksandria, 247/248) alikuwa askofu wa mji huo wa Misri tangu mwaka 231 hadi kifo chake.

Kabla ya hapo aliingia Ukristo kwa kuvutwa na kaka yake Plutarko na kwa kuwa kama yeye mwanafunzi wa Origen; hatimaye alimpokea katika uongozi wa chuo cha Aleksandria.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 4 Desemba[1][2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.