Errol Barnett (amezaliwa 3 Aprili 1983) ni mtangazaji na mwanahabari wa CNN International anayefanya kazi katika Makao Makuu ya CNN jijini Atlanta, Georgia. Yeye hutangaza habari za 'World Report' na pia ni mtangazaji mkuu wa 'iReport for CNN', ambacho ni kipindi cha CNN kinachoonyesha video, picha na hadithi zenye manufaa na zilizotengenezwa na "iReporters" wa CNN kutoka kote duniani.[1]

Errol Barnett

CNN International

hariri

Tangu alipojiunga na CNN mwaka 2008, Barnett amekuwa akitumia jamii hata akiripoti habari zenye umuhimu kama vita vya baada ya uchaguzi wa Iran; mabomu ya kigaidi mjini Jakarta; mtetemeko wa ardhi iliyotokea L'Aquila; ajali ya ndege ya Kituruki karibu na Amsterdam; na vita baina ya Israel na Gaza iliyotokea hapo mapema mwaka 2009.

Ametambulika kama "Power 30 Under 30" na Atlanta's Apex society. Ilihifadhiwa 10 Machi 2010 kwenye Wayback Machine. Barnett ametangaza habari za aina mbalimbali akiwa CNN kama vile maendeleo ya sheria ya kupambana na uharamia nchini Ufaransa na Uingereza; mtazamo wa watu kote duniani kuhusu kushinda kwa Rais wa Marekani, Barack Obama, Tuzo la Amani la Nobel 2009; na uchaguzi wa rais katika Israeli, Afghanistan na Afrika Kusini. Sehemu za taarifa za habari anazotangazwa zinapatikana kwa CNN.com

Historia

hariri

Errol alizaliwa mjini Milton Keynes, Uingereza, wazazi wake ni Pamela na Michael Christie. Yeye ana kaka mmoja, aitwaye Danny Christie. Mamake aliolewa na Gary Barnett baadaye, aliyekuwa akifanya kazi kama jeshi wa US Air Force, ambayo iko nchini Uingereza na baadaye alihudumu katika Vita vya Gulf. Familia yote ilihamia Phoenix, Arizona mwaka 1993.[2] Errol alihudhuria Shule ya Msingi ya Garden Lakes na Shule ya Upili ya Westview kabla ya kuajiriwa naChannel One News.

Channel One

hariri
Faili:ChannelOneAnchors2004.jpg
Channel One Anchors 2004: (kushoto na kulia) Janet Choi, Derrick Shore, Alexandra Panther, Errol Barnett, Yoshua Toole na Lauren Jiggetts

Kazi ya Barnett ya uandishi ilianza mwaka 2001 alipokuwa na umri wa miaka 18 na yeye alikuwa mwanahabari mdogo zaidi wa Channel One News. Katika miaka yake mitano aliyofanyia Channel One, Barnett alitangaza taarifa mbalimbali kama "Democratic National Convention" ya 2004; mashambulizi ya 11 Septemba 2001; dhoruba za Ivan na Lily; uzinduzi wa pili wa Rais Bush; [[na moto mkali uliyotokea mjini California.|; na moto mkali uliyotokea mjini California.]] Barnett pia alitoa taarifa kuhusu matumizi ya dawa ya kulevya ya heroin katika vitongoji vya Marekani.

Ripoti zingine za kisiasa alizotoa ni kama ripoti kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa pindi Katibu wa Jimbo la Marekani Colin Powell alipotoa taarifa za kutatanisha kuhusu silaha za maangamizi; ripoti nyingine ilitoka kwa Makao Makuu ya Marekani wakati wa kutolewa Homeland Security Act. [3] Barnett alipokea tuzo la Telly na alichaguliwa kwenye jarida la Teen People kama mmoja wa "vijana 20 watakao badilisha ulimwengu" kwa ajili ya kazi yake. Yeye aliwacha kazi Channel One mwaka 2006 baada ya kukubaliwa na UCLA kumaliza masomo yake ya shahada ya kwanza.

UCLA na ReelzChannel

hariri

Barnett alipokea shahada yake ya sanaa ya siasa kwa lengo la mahusiano ya kimataifa kutoka UCLA na alikuwa mwanachama wa Kappa Alpha Psi. Yeye aliwekwa kwenye gazeti la The Daily Bruin mwezi Aprili 2007 na kufuzu Juni 2008 Wakati alipokuwa mwanafunzi wa UCLA alifanya kazi kama mwanahabari na mtangazaji mkuu wa ReelzChannel. Mwezi Julai 2008 Barnett alitangaza kwenye "Dailies" kwamba amaondoka hapo na atajiunga na CNN International.

Marejeo

hariri
  1. CNN bio / CNN / anchors_reporters / barnett.errol.html
  2. "Teen Mtandao Best article". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-01-01. Iliwekwa mnamo 2009-12-17.
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-03-13. Iliwekwa mnamo 2009-12-17.

Viungo vya nje

hariri