Estrojeni

(Elekezwa kutoka Estrogeni)

Estrojeni (kutoka neno la Kiingereza "estrogen" lenye asili ya Kigiriki: οἶστρος, oistros, linaloweza kudokeza "hamu ya ngono" na kiambishi tamati γεν, gen, "sababishi") ni homoni ya kike muhimu zaidi ambayo imo mwenye mwili wa wanyama aina ya Chordata (wenye uti wa mgongo) na baadhi ya wadudu.

Katika binadamu, homoni hii ni muhimu hasa kwa wanawake na hutunzwa kwenye ovari, ini na huwasaidia wanawake wajawazito, huwasaidia wasichana kwenye ukuaji, husaidia pia kwenye kipindi cha ovulasheni. Wakati wa hedhi kwisha kabisa kiwango cha estrogeni hushuka.

Jina estrojeni pia linaweza kutumika kwa kitu chochote ambacho chaiga homoni hiyo kama vile dawa ambazo hupewa wanawake ili wawe na ashiki ya ngono.

Kazi ya estrojeni

hariri

Homoni ya estrojeni zikishirikiana na homoni ya ukuzi (human growth hormone) husaidia katika ubalehe wa wasichana ambapo matiti yao madogo yaanza kunenepa na kuwa makubwa. Estrojeni pia husaidia kufanya mafuta yagawanyike sawa katika msichana anayebalehe ili awe wa kuvutia na mwenye ngozi nyororo. Homoni hii pia huwafanya wasichana waanze kupata matako yaliyowanda.

Estrojeni hufanya uke wa msichana uwe umekomaa ili awe tayari kushiriki katika tendo la ndoa na pia kushika mimba. Homoni hii huwafanya wasichana wapate uchu wa ngono, au ashiki ya mapenzi na kwa njia hii huonekana kama homoni ya uzazi wa wanawake.

Estrojeni pia husaidia mama anapokuwa mjamzito ili matiti yake yawe tayari kutoa maziwa ya kunyonyesha mtoto

Estrojeni na tesistosteroni

hariri

Kinyume cha homoni ya estrojeni ni homoni ya tesistosteroni ambayo inapatikana sanasana kwa wanaume. Hata hivyo, wanawake wana kiwango fulani cha tesistosteroni ilhali wanaume nao wana kiwango fulani cha estrojeni. Tofauti ni kwamba wanawake wana estrojeni nyingi zaidi mwilini ikilinganishwa na tesistosteroni ilhali wanaume nao wana kiwango kikubwa cha tesistosteroni ikilinganishwa na estojeni.

Mtoto mchanga anapozaliwa, awe wa kiume au kike, huwa na estrojeni nyingi sana mwilini na ndiyo maana huwa na jinekomastia. Hii hufanyika maana homoni ya estrojeni hutoka kwa mama mzazi hadi kwa mtoto. Jinekomastia hiyo huisha mtoto anapozaliwa na kukaa kwa muda.

Jinekomastia pia hupatikana kwa wanaume walio na umri wa miaka thelathini kwenda juu wanapokuwa na estrojeni nyingi mwilini. Ili kumaliza matiti haya, hushauriwa wanywe dawa za kuongeza tesistosteroni mwilini au wafanywe upasuaji wa liposuction au mastectomy ili ufuta uliokuwa katika matiti haya utolewe.

  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Estrojeni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.