Eulogi wa Edessa (alifariki 23 Aprili 387) alikuwa askofu wa Edessa, leo Urfa, nchini Uturuki.

Alipokuwa padri alifukuzwa kutokana na dhuluma ya kaisari Valens, aliyekuwa Mwario, dhidi ya Wakatoliki, akaishi Antinoe, Misri.

Kaisari huyo alipofariki, Eulogi alirudi kwao akafanywa askofu wa jimbo akaliongoza kwa bidii hadi kifo chake klilichotokea siku ya Ijumaa Kuu [1].

Alishiriki Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli (381).

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Aprili[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/50560
  2. Martyrologium Romanum, 2004
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.