Fernando Perez na Alois Blanc

Fernando Perez na Alois Blanc (waliuawa 1250) walikuwa walei wa utawa wa Wamersedari kutoka Hispania waliotumwa Tunis kukomboa watumwa lakini baharini walikamatwa na maharamia Waturuki.

Baada ya kuporwa pesa za kukombolea watumwa, waliagizwa kukana imani yao, lakini walikataa katakata. Kwa sababu hiyo, kisha kuteswa sana, walitupwa majini wakiwa wamefungiwa mawe makubwa shingoni [1].

Sikukuu ya hao watakatifu wafiadini huadhimishwa shirikani tarehe 16 Oktoba.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.