Mkuyu

(Elekezwa kutoka Ficus)
Mkuyu
(Ficus spp.)
Mkuyu mwangajo (Ficus sur)
Mkuyu mwangajo (Ficus sur)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Rosales (Mimea kama mwaridi)
Familia: Moraceae (Mimea iliyo na mnasaba na mforosadi)
Jenasi: Ficus
Röding
Ngazi za chini

Kadiri ya spishi 800

Mikuyu ni miti ya jenasi Ficus. Kwa kawaida hiyo ni miti mikubwa. Maua, na hivyo matunda pia, huota kutoka shina na matawi makubwa. Matunda huitwa makuyu.

Kuna kadiri ya spishi 800 za mikuyu. Mkuyu unaopandwa na ambao matunda yake huliwa sana, una jina lake: mtini, na matunda yake matini.

Makuyu si matunda halisi. Tabaka la nje ni sehemu ya tawi iliyojifunga katika tufe na huitwa sikonio (syconium). Mkabala na kikonyo kuna tundu dogo liitwalo ostioli. Maua yamo upande wa ndani wa ukuta wa sikonio. Uchavushaji wa maua hufanyika na nyigu wadogo sana (nyigu-makuyu). Jike la nyigu, ambao ametoka kwenye sikonio nyingine na amepambwa na chavua, aingia kupitia tundu dogo kwa nguvu akipoteza mabawa yake. Halafu ataga mayai katika ovari za maua na sawia achavusha stigma. Baada ya kutoka kwenye mayai lava wala tishu za maua. Madume wakiwa wamekuwa wapevu hawana mabawa na wapanda majike tu. Halafu watoboa tundu katika sikonio ili kuacha majike watoke na baadaye madume wafa. Kila spishi ya mkuyu ana spishi yake (au zake) ya (za) nyigu maalum.

Katika Biblia hariri

Nabii Amosi alikuwa analima mikuyu (Am 7:12-15), lakini mti huo umepata umaarufu kutokana na Zakayo kupanda juu yake ili kumuona Yesu akipita mjini Yeriko (Lk 19:1-10).

Spishi zilizochaguliwa hariri

Picha hariri