Fidensyani, Valeriana, Viktorya na wenzao
Fidensyani, Valeriana, Viktorya na wenzao kumi na saba (waliuawa Hippo, leo Annaba nchini Algeria, 304) ni wafiadini waliosifiwa na Augustino wa Hippo kwa imani yao na ushindi wao katika mateso [1].
Fidensyani alikuwa askofu wa Hippo kuanzia mwaka 303 hadi kifodini chake mwaka uliofuata.
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 15 Novemba[2][3].
Inawezekana watakatifu Fidensyani, Sekundo, Variko na wenzao wanaoheshimiwa siku hiyohiyo[4] na watakatifu Bariko, Donati, Honorati, Januari, Marko, Paulo, Rufino, Valeri, Vikta, Vitalis na Yusto wanaoadhimishwa kesho yake[5], si makundi mengine.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |