For a Few Dollars More
For a Few Dollars More (kwa Kiitalia: Per qualche dollaro in più) ni filamu ya mwaka wa 1965 ya Kiitalia-Kihispania ya spaghetti western ambayo imeongozwa na Sergio Leone. Ndani yake anakuja Clint Eastwood, Lee Van Cleef na Gian Maria Volonté wakiwa kama nyota wakuu wa filamu hii.[1] Mwigizaji wa Kijerumani Klaus Kinski amecheza kama mwigizaji msaidizi katika upande wa maadui. Filamu ilitolewa nchini Marekani kunako mwaka wa 1967 na ni ya pili katika kile kisa kinajulikana kwa jina la Trilojia ya Dollars.
For a Few Dollars More (Per qualche dollaro in più) | |
---|---|
Imeongozwa na | Sergio Leone |
Imetayarishwa na | Arturo González Alberto Grimaldi |
Imetungwa na | Hadithi: Sergio Leone Fulvio Montella Mchezo: Sergio Leone Luciano Vincenzoni |
Nyota | Clint Eastwood Lee Van Cleef Gian Maria Volonté Klaus Kinski |
Muziki na | Ennio Morricone |
Imesambazwa na | United Artists |
Imetolewa tar. | Italia: 18 Novemba 1965 Marekani: 10 Mei 1967 |
Ina muda wa dk. | 132 |
Nchi | Italia Hispania |
Lugha | Kiitalia |
Bajeti ya filamu | $600,000 (makad.) |
Ilitanguliwa na | A Fistful of Dollars |
Ikafuatiwa na | The Good, the Bad and the Ugly |
Hadithi
haririEastwood (anatambulika kama "Man with No Name") na Van Cleef (kama Colonel Douglas Mortimer na anatambulika kama "Man in Black") wanacheza kama wakamata watoro wanaomwinda "El Indio" (Gian Maria Volonté), ni mmoja kati ya watoro wanaotafutwa sawana katika maeneo ya western, na kundi lake la kijambazi (mmoja katika hao kacheza Kinski).
Indio ni mkatili mno, mtu mwenye maarifa ya juu. Ana saa ya muziki ambayo anaichezesha kwanza kabla hajaingia kwenye mashindano ya kutandikana bunduki. "Wakati sauti ya kengere inaisha, anaanza," anasema. Kumbukumbu za awali zinaonyesha kwamba ile saa inatoka kwa msichana mdogo (Rosemary Dexter), ambaye amejiua baada ya kubakwa na Indio alipomkuta na mpenzi wake (katika utunzi wa riwaya ya Joe Millard wa filamu, bwana mdogo huo ni mumewe aliolewa naye karibuni) na akamwulia mbali. Saa imebeba picha ya mwanamke na ilitolewa kama zawadi kutoka kwa bwana mdogo kabla hajauawa.
Filamu inaaza na Colonel Mortimer (Cleef) anasimamisha gari moshi kwa njia isiyo-halali huko mjini Tucumcari, na punde baada ya kupokea mshahara wake wa uwindaji $1,000 juu ya Guy Calloway (José Terrón). Uwezo wake wa kutumia Mortimer unaonekana jinsi anavyomwua mtu kwa mbali kiubwete. Baada ya kupokea ujira wake hapohapo akaulizia kuhusu Red "Baby" Cavanagh (José Marco), ambaye ujira wake unalipwa $2,000, na alionekana mara mwisho mjini White Rocks.
Mortimer anaambiwa kama kwamba Cavanagh tayari keshakamatwa na Eastwood, ambaye anajulikana kama "Manco" (ina-maana mtu mmoja mwenye silaha kwa Kihispania — tazama maelezo chini). Tunamwona Manco akiingia mjini kumsaka Cavanagh kwenye kaukumbi cha wacheza kamaili. Manco anamwua jamaa na watu zake, na kumchukua mtafutwa huyo. Hatimaye, wasakaji watoro wawili, baada ya kujua vilivyo kutoka katika vyanzo tofauto, wanakutana mjini El Paso na, na kuzingua, akaamua kujiunga na lile kundi la majambazi wa Indio.
Lengo kuu la Indio ni kuiibia Benki ya El Paso na sefu yake ya uongo iliyojaa "mamilioni ya madola." Mortimer anamfuatilia Manco kiubishi na kujiunga na kundi la Indio wakati wa wizi wa benki ilimradi "awashe moto baina yao." Manco amepewa uanachama kundini baada ya kumwokoa mmoja kati ya wanakundi wa Indio jela.
Wakati anaiibia benki, kapeleka kundi la majambazi na fedha mpakani mwa mji mdogo wa Agua Caliente, ambapo Mortimer anakutana na Manco. Mshirika mwingine Wild (Klaus Kinski) amemtambua Colonel tangu katika shambulio la awali ambalo Colonel amemkutana kwa makusudi na kumlazimisha wapambane ambapo aliuliwa na Colonel. Yule Colonel amejithibitisha kama anathamani kwa Indio kwa kufungua lile sefu bila kutumia milipuko, lakini Indio ameeleza nia yake ya kusubiri mwezi iwapo watalazimika kupitisha mgao au wasubiri vuguvugu la wizi wa benki liishe au wazifungie zile pesa na wajikatae.
Manco na Colonel wanapiga hesabu ya kuiba zile pesa walizoiba benki kutoka mikononi mwa Indio, lakini wale vibaka wakawakamata na kuwapa kichapo cha haja. Mtu wa karibu wa Indio Nino (Mario Brega), amepewa agizo kutoka kwa Indio, kuuwa walinzi wao na kuwatoa wale wauwaji wa malipo. Indio anafahamisha kundi lake kwamba "wametoweka," na kuwatuma kuwakimbiza wale wauaja wa malipo waliotoroka. Amenuia kuuwa kundi lake lote kwa kutumia wauwaji wa kulipwa huku yeye na Nino wakichukua mgao wa pesa kivyao. Hata hivyo, yule mjanjarukaji Groggy (Luigi Pistilli) ametambua nia thabiti Indio, na kumwua Nino. Kabla hajamuua Indio, amekuta Colonel keshaondoa pesa zote zilizoibiwa na Indio katika mahali ambapo alificha. Indio anamshawishi Groggy kuunga vikosi ili wawatie nguvuni wale wauaji wa kulipwa.
Asubuhi yake, Manco na Mortimer wakatandika risasi lile kundi, mmoja baada ya mwingine, mule mitaani mwa mjini pale. Kubaki mpweke, Mortimer anamtandika risasi Groggy wakati kila mmoja anakimbilia hilo, halafu bunduki yake ikipigwa kutoka mkononi mwake na Indio, ambaye alichukua kifuko-cha-saa yake na kuanza kupiga mlio. Wakati mlio unaishia, Manco akatokea ghafla akiwa na kifuko-cha-saa aina ileile, kinachopiga mlio uleule kama wa Indio, ambapo Mortimer anagundua kama kilichukuliwa kwake hapo awali.
Wakati hili linatokea, Manco ameshika bunduki ya Henry kwa Indio na kutoa mkanda wa bunduki na pistol yake kwa Mortimer, dalili ya kushindwa. "Sasa tunaanza," Manco anatangaza na kukaa wakati Mortimer na Indio wanatoa macho. Wakati wa kusimama kidete, Manco anatazama chini ya kifuko-cha-saa na kumuona mwanamke yuleyule ambaye Indio alimbaka. Muziki unaishia, na Mortimer anafyatua risasi kwa Indio.
Katika njia panda hii, Mortimer anachukua kifuko-cha-saa cha Indio. Manco anamrudishia ile saa nyingine na kuashiria ufanani wa kifamilia; Colonel anajibu, "Kawaida, baina ya kaka na dada," inaonesha ya kwamba yule binti mdogo alionekana picha yaka pale ni mdogo wa Mortimer. Kisasi chake kimekamilika, na kuamua kutochukua hata punje ya malipo ya mauaji. Wakati Manco anatupa miili ya mwisho katika kigali cha farasi na kuwahesabu na kutoa zawadi kwa kila mmoja, anagundua kwamba kama amepungukiwa na jumla ya kiasi cha $27,000, na kuelekezea bunduki yake kwa Groggy ambaye ameponyeka na kusubiria katika shambulizi. Akiwa anaondoka, amepata zile pesa zilizoibiwa kutoka katika benki ya El Paso, ingawa haikuwa wazi kama anania ya kurejesha au la. Halafu anaonekana akipotea kwa mbali na farasi wake huku akivuta kigali cha farasi kilichojawa na miili iliyokosa maisha ya kundi zima la majambazi.
Washiriki
haririViongozi
hariri- Clint Eastwood kama Manco ("Blondie") ("The Man with No Name")
- Lee Van Cleef kama Colonel Douglas Mortimer
- Gian Maria Volonté kama El Indio ("The Indian")
Kundi la majambazi
hariri- Luigi Pistilli kama Groggy, mwanachama wa kundi la Indio
- Klaus Kinski kama Juan Wild, mwanachama wa kundi la Indio
- Benito Stefanelli kama Huey (aka Luke), mwanachama wa kundi la Indio[2]
- Mario Brega kama Niño, mwanachama wa kundi la Indio
- Aldo Sambrell kama Cuchillo, mwanachama wa kundi la Indio
Wahusika wengine
hariri- Dante Maggio kama Carpenter ndani ya selo akiwa na El Indio
- Diana Rabito kama msichana wa Calloway ndani yatub
- Giovanni Tarallo kama mwanatelegrafia Santa Cruz
- Joseph Egger kama Old Prophet
- Lorenzo Robledo kama Fred, msaliti wa El Indio
- Mara Krupp kama Mary, mke wa meneja wa hoteli
- Mario Meniconi kama Konda wa Treni
- Roberto Camardiel kama karani Stesheni
- Sergio Mendizábal kama meneja wa benki ya Tucumcari
- Tomás Blanco kama sheriff wa Tucumcari
Marejeo katika vyombo vya habari vingine
hariri- Lando Buzzanca parodied the film in For a Few Dollars Less.[3][4]
Tanbihi
hariri- ↑ Variety film review; 16 Februari 1966, page 6.
- ↑ Sergio Leone Web Board. Retrieved on 26 Januari 2010.
- ↑ http://www.youtube.com/watch?v=NBzBfFZUyoU&feature=related
- ↑ [shorturl.at/ozFX3 | For a Few Dollars More movie review (1967)]
Viungo vya Nje
hariri- For a Few Dollars More katika Internet Movie Database
- (Kiingereza) For a Few Dollars More katika Allmovie
- For a Few Dollars More at the TCM Movie Database
- For a Few Dollars More Ilihifadhiwa 24 Mei 2011 kwenye Wayback Machine. at the Spaghetti Western Database
- For a Few Dollars More katika Rotten Tomatoes