Fransisko Antoni Fasani

(Elekezwa kutoka Fransisko Antonio Fasani)

Fransisko Antoni Fasani (Lucera, 6 Agosti 1681 - Lucera, 29 Novemba 1742) alikuwa padri wa utawa wa Ndugu Wadogo Wakonventuali kutoka Italia Kusini.

Msomi mkubwa, alipenda sana kuhubiri na kufanya toba, pamoja na kuhurumia fukara na wenye shida yoyote kwa kutoa daima bila kusita hata mavazi yake kuvika ombaomba na kuwapa wote msaada wake wa Kikristo [1].

Alitangazwa na Papa Pius XII kuwa mwenye heri tarehe 15 Aprili 1951, halafu tarehe 13 Aprili 1986 Papa Yohane Paulo II alimtangaza kuwa mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.