Fuko (mnyama)
Fuko | ||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Fuko wa Damaraland (Fukomys damarensis)
| ||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||
|
Mafuko ni wanyama ambao wanachimba katika ardhi na kushinda takriban maisha yao yote chini ya uso wake. Wanyama hawa wamo katika oda na familia mbalimbali. Spishi za Afrika zimo katika oda za Afrosoricida (familia Chrysochloridae) na Rodentia (familia Bathyergidae na Spalacidae). Oda Soricomorpha ina spishi katika Afrika, lakini hizi ni wanafamilia wa Soricidae (virukanjia). Mafuko wa Soricomorpha ni wanafamilia wa Talpidae, familia isiyokuwapo katika Afrika, lakini wanyama hawa wanatokea Asia, Amerika na Ulaya. Kuna spishi mbili huko Australia ambazo ni mamalia wanaobeba watoto wao wachanga ndani ya pochi (Notoryctidae). Mafuko wa Notoryctidae, Chrysochloridae na Talpidae hula nyungunyungu na wadudu, lakini wale wa Bathyergidae na Spalacidae hula mizizi, matunguu na viazi.
Picha
hariri-
Fuko-pochi
-
Fuko-dhahabu
-
Fuko uchi
-
Fuko-mwanzi
-
Fuko wa Ulaya