Kirukanjia (mamalia)

Kirukanjia
Kirukanjia rangi-mbili (Crocidura leucodon)
Kirukanjia rangi-mbili (Crocidura leucodon)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Soricomorpha (Wanyama kama virukanjia)
Familia: Soricidae
G. Fischer, 1817
Ngazi za chini

Nusufamilia 3:

Virukanjia au sange ni wanyama wadogo wanaofanana na vipanya wenye pua refu, lakini wanyama hawa si wagugunaji (oda Rodentia) na hula wadudu na nyungunyungu hasa lakini mbegu na makokwa pia na spishi kadhaa hukamata samaki wadogo. Meno yao yamechongoka yenye ncha kali. Virukanjia ni wadogo sana. Spishi kubwa kabisa ina sm 15 na uzito wa g 100; ile ndogo kabisa ina sm 3.5 tu na uzito wa g 2 (Kirukanjia wa Etruski, mamalia wa ardhi mdogo kabisa duniani). Rangi yao ni nyeusi, kijivu au kahawia.