Open main menu
Furukombe
Furukombe wa Afrika
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Accipitriformes (Ndege kama vipanga)
Familia: Accipitridae (Ndege walio na mnasaba na vipanga)
Nusufamilia: Haliaeetinae (Ndege walio na mnasaba na furukombe)
Jenasi: Haliaeetus Savigny, 1809

Ichthyophaga Lesson, 1843

Furukombe, fukombe, kwazi, yowe au tai mlasamaki ni ndege mbua wa nusufamilia Haliaeetinae katika familia Accipitridae. Ndege hawa ni baina ya tai wakubwa kabisa. Uzito wao unatofautiana kutoka kg 2 (furukombe wa Sanford) mpaka 9 (furukombe wa Steller). Manyoya yao yana rangi ya kahawa mpaka nyeusi lakini kichwa, mkia, kidari na tumbo ni nyeupe kufuatana na spishi. Furukombe wa Madagaska, wa Sanford na wa Ulaya wana kichwa hudhurungi. Spishi zote zinatokea karibu na maji ama baridi au ya bahari. Hula samaki hasa lakini ndege wengine, mizoga na mara kwa mara wanyama wadogo pia. Hujenga tago lao kwa vijiti juu ya mti au mwamba. Jike hutaga mayai 1-3.

Spishi za AfrikaEdit

Spishi za mabara mengineEdit

PichaEdit