Kanu (mnyama)
Kanu | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kanu madoa-madogo (Genetta genetta)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Spishi 14:
|
Kanu, kala au karasa ni wanyama wadogo wa jenasi Genetta katika familia Viverridae. Kanu mlasamaki aliainishwa katika jenasi Osbornictis lakini wataalamu wameonyesha kama spishi hii ina mnasaba wa karibu na kanu wa jenasi Genetta. Wanyama hawa ni warefu na wembamba wenye mkia mrefu, kichwa kidogo na masikio makubwa. Rangi yao ni nyeupe hadi njano na wana madoa meusi na mkia wenye miviringo. Mkia wao ni mrefu sana: 1-1.5 mara urefu wa mwili. Hiyo inawapa taraju wakisombea miti na kuchupa matawi. Wanatokea Afrika tu isipokuwa kanu madoa-madogo ambaye anatokea Rasi ya Iberia na Mashariki ya Kati pia. Kanu wana tezi kando ya mkundu zinazotoa aina ya zabadi ambayo inanuka sana. Hula wanyama wadogo, mijusi, ndege wadogo, amfibia, wadudu na hata matunda.
Spishi
hariri- Genetta abyssinica, Kanu Habeshi (Abyssinian Genet au Ethiopian Genet)
- Genetta angolensis, Kanu-miyombo (Angolan Genet au Miombo Genet)
- Genetta bourloni, Kanu wa Bourlon (Bourlon's Genet)
- Genetta cristata, Kanu Ushungi (Crested Genet) - wataalamu wengine wanafikiri kwamba hii ni nususpishi ya Genetta servalina
- Genetta genetta, Kanu Madoa-madogo (Common Genet, European Genet au Small-spotted Genet)
- Genetta johnstoni, Kanu wa Johnston (Johnston's Genet)
- Genetta maculata, Kanu Madoa-kutu (Rusty-spotted Genet au Panther Genet)
- Genetta pardina, Kanu Madoa-makubwa Maghribi (Pardine Genet au West African Large-spotted Genet)
- Genetta piscivora, Kanu Mlasamaki (Aquatic Genet) – pengine inaainishwa katika jenasi Osbornictis
- Genetta poensis, Kanu Mfalme (King Genet)
- Genetta servalina, Kanu-mondo (Servaline Genet)
- Genetta thierryi, Kanu Hausa (Haussa Genet au Thierry's Genet)
- Genetta tigrina, Kanu Madoa-makubwa Kusi Cape Genet, Blotched Genet au South African Large-spotted Genet)
- Genetta victoriae, Kanu Mkubwa (Giant Genet)
Picha
hariri-
Kanu-miyombo
-
Kanu-mondo
-
Kanu madoa-makubwa kusi
Marejeo
haririWikispecies has information related to: Genetta |