Kanu (mnyama)

(Elekezwa kutoka Osbornictis)
Kanu
Kanu madoa-madogo (Genetta genetta)
Kanu madoa-madogo (Genetta genetta)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Carnivora (Wanyama mbua)
Nusuoda: Feliformia (Wanyama kama paka)
Familia: Viverridae (Wanyama walio na mnasaba na paka zabadi)
Nusufamilia: Viverrinae (Wanyama wanaofanana na paka zabadi)
Jenasi: Genetta
Oken, 1816
Ngazi za chini

Spishi 14:

Kanu, kala au karasa ni wanyama wadogo wa jenasi Genetta katika familia Viverridae. Kanu mlasamaki aliainishwa katika jenasi Osbornictis lakini wataalamu wameonyesha kama spishi hii ina mnasaba wa karibu na kanu wa jenasi Genetta. Wanyama hawa ni warefu na wembamba wenye mkia mrefu, kichwa kidogo na masikio makubwa. Rangi yao ni nyeupe hadi njano na wana madoa meusi na mkia wenye miviringo. Mkia wao ni mrefu sana: 1-1.5 mara urefu wa mwili. Hiyo inawapa taraju wakisombea miti na kuchupa matawi. Wanatokea Afrika tu isipokuwa kanu madoa-madogo ambaye anatokea Rasi ya Iberia na Mashariki ya Kati pia. Kanu wana tezi kando ya mkundu zinazotoa aina ya zabadi ambayo inanuka sana. Hula wanyama wadogo, mijusi, ndege wadogo, amfibia, wadudu na hata matunda.

Spishi

hariri

Marejeo

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: