Gentile wa Fabriano

(Elekezwa kutoka Gentile da Fabriano)

Gentile wa Fabriano (1370 hivi – 1427) alikuwa mchoraji wa Italia aliyefanya kazi hasa katika mkoa wa Toscana.

Ibada ya Mamajusi (1423)
Bikira Maria katika Ibada ya Mamajusi (1423).

Michoro yake maarufu zaidi inawahusu Yesu na Bikira Maria, nayo ni Ibada ya Mamajusi (1423) na Kukimbilia Misri.

Maisha

hariri

Gentile alizaliwa Fabriano, katika dola la Papa, (leo mkoa wa Marche).

Kabla ya mwaka 1380 mama yake alifariki, na hapo baba yake, Niccolò di Giovanni Massi, alijiunga na monasteri, alipofariki mwaka 1385. Hakuna habari zaidi kuhusu malezi yake.

Mwaka 1405 hivi, Gentile alikuwa akifanya kazi huko Venice, halafu akachora huko Fabriano, Foligno, Brescia, halafu tena Fabriano.

 
Bikira Kutiwa Taji

Tarehe 6 Agosti 1420 alikuwa Florence, halafu Siena, Orvieto na hatimaye mwaka 1427 alifika Roma, alipopata agizo la Papa Martin V, lakini hakumaliza kulitekeleza kwa sababu alifariki kabla ya tarehe 14 Oktoba.

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • Mack, Rosamond E. Bazaar to Piazza: Islamic Trade and Italian Art, 1300–1600, University of California Press, 2001, ISBN 0-520-22131-1
  • Gentile da Fabriano e l'altro Rinascimento, catalogo della mostra (Fabriano, 21 aprile-23 luglio 2006), Electa, 2006.
  • Fabio Marcelli, Gentile da Fabriano, Silvana, 2005.
  • Andrea De Marchi, Gentile da Fabriano. Un viaggio nella pittura italiana alla fine del gotico, Federico Motta, 2006 (I ed. 1992).

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gentile wa Fabriano kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.