GeorDavie
GeorDavie (alizaliwa Singida, 25 Aprili 1965) ni nabii, mwanamuziki, mwandishi, mfadhili, tena mwanzilishi na kiongozi mkuu wa kanisa la Ngurumo ya Upako [1].
GeorDavie | |
---|---|
Taarifa za awali | |
Jina la kuzaliwa | GeorDavie |
Amezaliwa | 25 Aprili 1965 |
Kazi yake | Nabii |
Ndiye mwandishi wa kitabu “Keeping Up With God’s Kingdom Government Standards”.
Historia
haririMaisha na elimu
haririGeorDavie [2] alizaliwa na Moses Kasambale, daktari wa binadamu, na Phoebe. GeorDavie ana asili ya Kisomali, Kiarabu na Kiitalia.
GeorDavie alikulia Singida na baadaye akahamia jijini Dar es Salaam kuishi na baba yake mzazi. Wazazi wake waliishi katika miji tofauti hivyo alihama mara kwa mara alipokuwa mdogo. Bibi yake Mary ni kati ya watu waliomlea. Akiwa na miaka mitano tu alianza kutoa unabii nao ulitimia kama alivyosema.
GeorDavie alipata elimu ya sekondari katika shule ya Minaki. Baadaye alikwenda Mombasa kusomea umisionari katika chuo cha Youth With A Mission (YWAM) na kuanza safari yake ya utume mwaka 1986.
Kutoka mwaka 1995 hadi 2012 alifanya mafunzo ya utumishi kutoka kituo cha Destiny Christian kilichopo Burnsville, Minnesota. Alialikwa kuhudumia kama mtumishi Oakland, California na kwenye miji pacha ya Minnesota wakati wa mafunzo yake. Mwaka 2013 GeorDavie alipata shahada ya PhD kwa njia ya mtandao kutoka chuo cha American University.
Maisha binafsi
haririMwaka 1988 GeorDavie alimuoa Anna Davie wakapata watoto watatu, Nic [3], Ken na Monica. Mke wake Anna Davie ni Mchungaji Kiongozi wa kanisa lake GeorDavie Ministries International – Ngurumo Ya Upako.
Muziki
haririSafari ya muziki ya GeorDavie ilianza alipokuwa na miaka sita, mama yake alipompatia zawadi ya gitaa. Alijifunza mwenyewe jinsi ya kucheza gitaa. Wakati akiwa shule aliendeleza kipawa chake cha muziki kwa kuanzisha vikundi vya kusifu. Mwanzoni mwa miaka ya 1980 ndipo alipoanza kurekodi muziki wake kwenye kaseti za redio. Aliendelea kujifunza namna ya kucheza vyombo mbalimbali vya muziki na staili yake ya kuimba ilidumu kuonekana ya pekee.
Baada ya kumaliza masomo yake GeorDavie alihamia Arusha kuanzisha kanisa na kuendelea na muziki. Alipokuwa huko alianzisha bendi ya muziki iliyoitwa Fishers Band na kufungua studio ya kurekodi, The Grand House of Supreme Music. Katika hiyo studio ndiye aliyekuwa mhandisi wa kurekodi. Alikuwa akirekodi wanamuziki mbalimbali, kwaya na bendi kutoka Afrika ya Mashariki.
Mwaka 1992 alifanya tamasha lake la kwanza ambalo pia lilikuwa tamasha la kwanza la muziki wa Injili Tanzania. aziri wa Mambo ya Ndani Augustine Lyatonga Mrema alikuwa mgeni rasmi wa tamasha hilo.
GeorDavie [4] hajawahi kuuza muziki wake. Aliwahi kusema kwenye moja ya mahojiano yake kwamba anafanya muziki kwa ajili ya ufahari wa serikali tukufu ya ufalme wa Mungu. Ijapokuwa kwa sasa anajihusisha zaidi na utumishi, bado anafanya muziki kimyakimya na bendi yake GeeDee SKY Jazz. Jina lake akiwa jukwaani ni Maestro GeeDee.
Huduma/Kanisa
haririSafari yake ya utumishi [5] ilianza mwaka 1980. Baada ya kumaliza masomo yake alitumika kama mtume Tanzania, Kenya na Uganda.
Mwaka 1991 alianza kufanyia kazi maono ya huduma yake ya Global Concert Church/GeorDavie Ministries International – Ngurumo ya Upako. Alisajili huduma hiyo mwaka 1994. Hiyo ilianza kama huduma ya kuunganisha waimbaji wa muziki wa Injili wa Afrika Mashariki, kuhubiri na kufundisha neno la Mungu makanisani na kusaidia watoto wa mitaani.
Mwaka 1995 alipata maono ya kuanzisha redio na mwaka 1997 alipata kisambazaji cha redio kidogo cha wati 100. Kisambazaji hicho kilimuwezesha kufikia watu waliokuwa karibu na eneo alilokuwa akirusha vipindi vyake. Mwaka 2012 alisajili rasmi redio yake ya Ngurumo Ya Upako FM. Mwaka 2018 alianzisha televisheni yake ya GeorDavie TV.
Novemba 14, mwaka 1999 ndio ilikuwa mwanzo rasmi wa kanisa la GeorDavie Ministries – Ngurumo Ya Upako ambalo kwa wakati huo lilijulikana kama kanisa la Destiny. Kanisa hilo lilianzia sebuleni mwake. GeorDavie aliwahi kusema kwamba kwa wakati huo alikuwa hajaamua ataita nini kanisa lake, lakini aliliita Destiny (Kanisa la Uelekeo) akijua na kumaanisha moyoni mwake kwamba kuna mahali anakwenda. Atakapokaribia anapokwenda atajua jina rasmi la kuita kanisa lake. Mwaka 2003 alibadilisha jina la kanisa na kuliita Ngurumo Ya Upako [6].
Kati ya mwaka 2005 hadi 2011 Mungu alimuongoza GeorDavie kufanya mikutano mikubwa [7] [8] na ya kihistoria ndani na nje ya nchi. Ikiwa ni pamoja na kufungua matawi ya kanisa Dar es Salaam[9], Mwanza, Mbeya, Morogoro, Manyara, Kilimanjaro, Congo na Marekani. Arusha ikiwa ndio makao makuu ya kanisa ulimwenguni na ikulu ya nabii huyo. Lengo la mikutano hiyo lilikuwa kutambulisha huduma ya kinabii Tanzania kwa sababu ilikuwa ni huduma isiyojulikana. Kwa sasa kanisa lake huhudhuriwa na takriban watu 5,000 kila wiki na kupata wageni kutoka mikoa mbalimbali Tanzania na ulimwenguni kote.[10]
Uamsho Marekani
haririMwaka 2017 GeorDavie alifanya ziara ya kinabii nchini Marekani kwenye jimbo la California, mjini Los Angeles. Alifanya hiyo ziara kwa lengo la kuwasilisha neno alilokuwa amepewa na Mungu kuwa “Uamsho ni sasa”. Aliachilia neno hilo katika kanisa la Five-Fold ambalo awali lilijulikana kama kanisa la Advanced Anointing. Alimpaka mafuta Kathryn Krick [11] kuwa mtume na baadaye kumteua kuwa Mchungaji Kiongozi wa kanisa la Five-Fold. Mtume Kathryn Krick na kiongozi wa sifa (Jeanntal Marshall) walilishika hilo neno kwa uaminifu kwa takriban miaka minne hadi uamsho ulipoanza kuonekana huko Marekani mwanzoni mwa mwaka 2021. Uamsho huo umekuwa ukisambaa na kugusa watu wa mataifa mbalimbali na kuthibitisha neno lililosemwa na Nabii GeorDavie mwaka 2017.
Misaada
haririGeorDavie alianzisha kituo cha Lighthouse kwa ajili ya watoto wa mitaani. Pia alifanya jitihada za kutambua na kutatua changamoto ya watoto hao mjini Arusha, kanda ya kaskazini Tanzania, kwa kuwapatia chakula, mavazi, mahali pa kuishi na kuwalipia ada za shule.
Kila mwaka GeorDavie husaidia vituo vya watoto yatima na vituo vya wazee [12] kwa kuwapa chakula na mahitaji mengine muhimu. Faraja, Christian Women, Samaritan Village, Kindness children care na St. John ni kati ya vituo vya watoto yatima ambavyo GeorDavie hutoa msaada. Vilevile GeorDavie amesaidia makanisa mbalimbali kwa kuwaruzuku pesa taslimu, kuwajengea maabadi yao na kuwanunulia vyombo vya muziki. Amezawadia watu mbalimbali vyombo vya usafiri ambavyo hadi sasa vimezidi mia moja.[13]
Malaika Njiani
haririMwaka 2019, GeorDavie alianzisha programu inayoitwa Malaika Njiani ambayo yeye ndiye mfadhili. Lengo la programu hii ni kumruzuku pesa mtu yeyote anayepitia changamoto za maisha bila kujali dini wala kabila.
Mwaka 2022, GeorDavie alijikita zaidi kwenye kugusa maisha ya watu wenye uchumi wa chini kwa kuwasaidia mitaji na vyombo vya usafiri kama bajaji ili waweze kuendesha maisha yao. Inasemekana kiasi cha fedha alichotoa hadharani kwa watu mbalimbali mwaka 2022 ni TZS 600,000,000.
Hapo kwenye Kanisa la GeorDavie watu mbalimbali walianza kumuimbia, wengine wakijichora miili yao jina na picha ya GeorDavie, watu kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania wakibandika picha za GeorDavie kwenye bajaji zao, wengine wakichora rangi yenye bendera ya Ngurumo Ya Upako mwilini mwao na kutembea nayo kutoka Dar mpaka Arusha, huku wasanii wakubwa nchini Tanzania na nje ya mipaka yake kama Shamsa Ford, Halima Yahya (Davina), Christina Shusho, Kidum kutoka Kenya, Mkali Wenu, Bondia Shaban Kaoneka, Mr. Pimbi, 20 Percent, Dude pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali, akiwemo Mbunge wa Arusha mjini, Mrisho Gambo, Mbunge wa jimbo la Nsimbo, Anna Lupembe, wakijitokeza kumuongelea GeorDavie. Mambo hayo yote yalianza kujitokeza kwa ukubwa baada ya GeorDavie kugusa maisha ya watu wengi kwa kuwapa mitaji, magari, bajaji, kuwajengea nyumba.
GeorDavie alianza mwaka 2023 kwa kutoa TZS 100,000,000 kwa wafanyabiashara wadogowadogo wa soko la NMC Samunge lililopo Arusha.
Tuzo
haririNovemba 2022, GeorDavie alitunikiwa tuzo ya Ubalozi wa amani na taasisi iliyopo nchini Burundi inayoitwa Mandela Peace Center na hiyo ndiyo sababu ya kuitwa Balozi wa Amani.
Diskografia
haririHizi ni albamu na nyimbo zilizotayarishwa na kurekodiwa na GeorDavie
- TROUBLED MAN (2010)
- Troubled Man (2010)
- Lead Me Now (2010)
- He Loves You And Alright (2010)
- Nilikuwa Mgonjwa Sana (2010)
- Preach the Word (2010)
- Umenisamehe (2010)
- Yesu Anakuja (2010)
- Nakupenda Bwana/I Love You (2010)
- Nani Atawafundisha Watoto (2010)
- NGEPENDA (2000)
- Ninakushukuru (2000)
- Ngependa (2000)
- Eeh Bwana Uniguse (2000)
- Tutamuona (2000)
- NILIPOTEA MBALI (1997)
- Nilipotea Mbali (1997)
- He's Gonna Move (1997)
- Never Be Alone (1997)
- Ushuhuda Wangu (1997)
- Glory Hallelujah (1997)
- Mene Mene (1997)
- You Are Blessed - Interlude (1997)
- I Love You So Much/ NAKUPENDA (1997)
- In The Moment Like This (1997)
- WORSHIP ALBUM (2005)
- Haleluya Jehovah (2005)
- Naamini Katika Upako (2005)
- Naamini Haleluya (2005)
- I Love You So Much (2005)
- NAKUTARAJIA (2003)
- Ameniokoa/Saved my Soul (2003)
- Mimi Nasafiri (the last part) (2003)
- Go Ye (2003)
- Nakutarajia (2003)
- No Time (2003)
- Raha Ndani Ya Roho (2003)
- Tazameni Ndege (2003)
- Usipotee Njia (2003)
- You Know Me Better (2003)
- Siku Hizi Jamani (1986)
- Wakristo Tuwe Macho (1986)
- Hakuna muda wa kupoteza (1987)
- Hakuna Mungu Mwengine (1987)
- Nimeulizwa (1987)
- Tangu Sasa (1987)
- Sitapungukiwa na Kitu (1987)
- Nilijaribu Mambo Mengi (1987)
- Jesus Washes Me (1987)
- PRINCE OF PEACE (1995)
- Prince Of Peace (1995)
- Keep Up (1995)
- Never Pretend (1995)
- Peace Of Mind (1995)
- Tell Me/Wanna Know U (1995)
- You Are So Special (1995)
- THE FISHERS DAYLIGHT (1989)
- Now I'm Satisfied (1989)
- The Fishers Daylight (1989)
- Ukaludie Kaya (1989)
- Wamekuwepo Watu Wengi (1989)
Nyimbo ambazo GeorDavie ameimba na GeeDee SKY Jazz
- Raha Ndani Ya Roho (Remastered) (2016)
- Preach the Word (Remastered) (2016)
- Haleluyah Jehovah (Remastered) (2016)
- Unatembea Mahali hapa (2016)
- Yesu Anakuja (Remastered) (2016)
- Skylight (2016)
- Tell me (2018)
- One Day Morning (2019)
- Tãtã Wêtû (2019)
- U r so special (Remastered) (2019)
- Bwana Yu Mwema (2019)
- Mbelewele (2019)
- Acha Ukali Basi (2019)
- Nguvu (2019)
- Tuko Poa (2019)
- Nashukuru (2021)
Marejeo
hariri- ↑ GeorDavie Ministries International
- ↑ https://www.christianonlineservices.org/2021/05/the-major-prophet-geordavie-biography.html Ilihifadhiwa 26 Januari 2022 kwenye Wayback Machine. GeorDavie Biography (Septemba 05, 2021). Iliangaliwa January 26, 2022.
- ↑ http://hosannainc.blogspot.com/2012/02/mtoto-wa-nabii-geordavie-aitwaye-nisher.html Nisher amshukuru Baba yake (Februari 29, 2012). Iliangaliwa Januari 26, 2022.
- ↑ https://strictlygospel.wordpress.com/2012/04/18/mheshimiwa-geordavie-kuimba-nyimbo-za-injili Mhe. GeorDavie kuimba nyimbo za injili (Aprili 18, 2012). Iliangaliwa Januari 26, 2022.
- ↑ https://tulonge.ning.com/profiles/blogs/nabii-geordavie-awa-mtumishi-wa-kwanza-kununua-helkopta-kwa-ajili Ilihifadhiwa 26 Januari 2022 kwenye Wayback Machine. (Oktoba 2, 2012). Iliangaliwa Januari 26, 2022.
- ↑ https://4ghabari.wordpress.com/2021/03/21/watanzania-watakiwa-kujitia-nguvu-na-kuvaa-ujasiri-haswa-katika-kipindi-hiki/(Machi 21,2021). Iliangaliwa Januari 26,2022.
- ↑ https://shaabanmpalule.blogspot.com/2014/07/angalia-picha-za-maisha-ya-askofu.html (Julai 29, 2014). Iliangaliwa Januari 26, 2022.
- ↑ https://www.udakuspecially.com/2014/02/askofu-bilionea-atikisa-bongo.html (Februari 25, 2014). Iliangaliwa Januari 26, 2022.
- ↑ https://allafrica.com/stories/200808181117.html AllAfrica - Arusha Times(Agosti 16, 2008). Iliangaliwa Januari 26, 2022.
- ↑ https://somalatest.blogspot.com/2019/04/watanzania-dumisheni-amani.html WATANZANIA DUMISHENI AMANI (Aprili 23, 2019). Iliangaliwa Januari 26, 2022.
- ↑ https://bbcgossip.com/entertainment/apostle-kathryn-krick-height-weight-net-worth-age-birthday-wikipedia-who-nationality-biography/ Ilihifadhiwa 26 Januari 2022 kwenye Wayback Machine. Kathryn Krick Biography (Novemba 18, 2021). Iliangaliwa Januari 26, 2022.
- ↑ https://mtazamomedia.blogspot.com/2016/12/dr-geordaviejijengeeni-tabia-ya.html WATANZANIA JIJENGEENI TABIA YA KUTOA(Desemba 26, 2016). Iliangaliwa Januari 26, 2022.
- ↑ http://www.diramakini.co.tz/2021/12/nabii-mkuu-tanzania-dktgeordavie-ampa.html?m=1 NABII GEORDAVIE AMZAWADIA GOODLUCK GOZBERT MERCEDEZ BENZ Iliangaliwa Januari 26,2022.