George Herbert Walker Bush ( 12 Juni 1924 - 30 Novemba 2018) alikuwa Rais wa 41 wa Marekani kuanzia mwaka wa 1989 hadi 1993. Kaimu Rais wake alikuwa Dan Quayle.

George H. W. Bush


Makamu wa Rais Dan Quayle
mtangulizi Ronald Reagan
aliyemfuata Bill Clinton

tarehe ya kuzaliwa 12 Juni 1924 (1924-06-12) (umri 99)
ndoa Barbara Pierce (1945-2018)
watoto George W. Bush, rais wa 43 wa Marekani
signature
tovuti Presidential Library

Akijulikana kama George Bush aliwahi kuwa mbunge, balozi wa Marekani, mkuu wa mamlaka ya upelelezi CIA na makamu wa rais Ronald Reagan. Alikuwa mwanasiasa wa Chama cha Jamhuri cha Marekani (Republican).

Kipindi cha urais wa Bush kiliona kuporomoka kwa ukomunisti katika Urusi na Ulaya ya Mashariki na mwisho wa vita baridi. Alitafuta maelewano na viongozi wa Urusi na kukubali maungano ya Ujerumani. Alituma jeshi la Marekani kwenye uvamizi wa Panama mwaka 1989 uliompindua dikteta Manuel Noriega na kwenye vita dhidi ya Irak iliyowahi kushambulia Kuwait.

Mwana wake George Walker aliingia pia katika siasa akaendelea kuwa rais wa 43 wa Marekani.

Tazamia pia hariri

}}

  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu George H. Bush kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.