Ulaya ya Mashariki

Ulaya ya Mashariki ni sehemu ya mashariki ya bara la Ulaya lakini hakuna maelewano juu ya mipaka yake hasa upande wa magharibi.

Ulaya Mashariki kutoka angani.

Ulaya ya Mashariki kufuatana na Umoja wa Mataifa

hariri

Umoja wa Mataifa hujumuisha nchi zifuatazo humo:

Orodha hii imejumlisha nchi zote za Ulaya zilizokuwa sehemu za Umoja wa Kisovyeti au zilizoshikamana nao kisiasa hadi mwaka 1989 (isipokuwa Ujerumani ya Mashariki). Tatizo lake ni ya kwamba watu wa Poland, Hungaria, Ucheki na Slovakia zinajihesabu kuwa sehemu za Ulaya ya Kati.

 
Ukuaji wa Ukristo Ulaya.

Ulaya ya Mashariki kijiografia

hariri

Kijiografia mara zinatajwa humo nyingi nchi za Ukraine, Belarus, Moldova na sehemu ya Ulaya wa Urusi. Isipokuwa sehemu za kaskazini za Urusi huhesabiwa mara nyingi upande wa Ulaya ya Kaskazini.

Ulaya ya Mashariki kiutamaduni

hariri

Mara nyingi nchi zinazokaliwa na watu wenye lugha za Kislavoni huhesabiwa humo. Lakini kwa njia hii Romania na Hungaria si nchi za Ulaya ya Mashariki lakini Ucheki, Slovenia na Kroatia zimo. Kihistoria hata sehemu za Ujerumani zilikaliwa na Waslavoni, na Wasorbi katika mashariki bado hutumia lugha yao.

Hivyo kuna nji ya pili inayosema: Nchi zote zenye lugha za Kislavoni zilizoguswa hasa na Kanisa la Kiorthodoksi kama vile Urusi, Ukraine, Belarus.