Gerard Kuiper
'
Gerard Kuiper | |
---|---|
Gerard Kuiper (1905 - 1973) | |
Amezaliwa | 7 Desemba 1905 |
Amefariki | 23 Desemba 1973 |
Kazi yake | a mwanaastronomia kutoka nchini Uholanzi |
Gerard Peter Kuiper (Kiholanzi: Gerrit Pieter Kuiper; 7 Desemba 1905 – 23 Desemba 1973) alikuwa mwanaastronomia kutoka nchini Uholanzi aliyeendelea kuishi Marekani.
Maisha
Kuiper alizaliwa kwenye familia ya fundi cherahani katika kijiji cha Uholanzi ya kaskazini. Tangu 1924 alisoma astronomia kwenye Chuo Kikuu cha Leiden. Jan Oort alikuwa kati ya walimu wake. Baada ya kumaliza shahada ya uzamivu kwa tasnia kuhusu nyota maradufu mwaka 1933 akapata nafasi ya kazi kwenye paoneaanga pa Chuo Kikuu cha Kalifornia, Marekani. Baadaye alikuwa profesa kwenye Chuo Kikuu cha Chicago na Chuo Kikuu cha Arizona.
Kazi
Utafiti wake ulihusu hasa mfumo wa Jua letu. Aliweza kuthibitisha kuwepo kwa dioksidi ya kaboni katika angahewa ya sayari Mirihi (Mars). Alitambua pia angahewa za miezi ya sayari kadhaa kama vile kwenye Titan (mwezi wa Zohali), Miranda (mwezi wa Uranus) na Nereid (mwezi wa Neptuni).
Alitabiri kuwepo kwa ukanda wa asteroidi nje ya obiti ya Neptuni iliyothibitishwa baadaye na kupokea jina la Ukanda wa Kuiper kwa heshima yake.
Other websites
- media kuhusu Gerard Kuiper pa Wikimedia Commons
- Gerard Peter Kuiper: NASA KAO's Namesake Archived 13 Julai 2014 at the Wayback Machine.
- National Academy of Sciences Biographical Memoir