Jan Hendrik Oort (28 Aprili 1900 - 5 Novemba 1992 [1]) alikuwa mwanaastronomia kutoka nchini Uholanzi aliyeweka misingi muhimu ya kuelewa galaksi yetu.

Jan Hendrik Oort (1900 - 1992).

Alitajwa kuwa mmoja wa wanaastronomia muhimu zaidi wa karne ya 20[2] [3]. Wingu la Oort, kwenye sehemu za nje za mfumo wa Jua, lilipewa jina lake.

Maisha

Oort alisoma kwenye Chuo Kikuu cha Groningen. Tangu mwaka 1924 alifanya kazi kwenye paoneaanga mjini Leiden. Tangu mwaka 1945 hadi 1970 alikuwa profesa kwenye Chuo Kikuu cha Leiden pamoja na kuwa mkurugenzi wa paoneaanga.

Utafiti

Anakumbukwa kwa utafiti wake kuhusu tabia za Njia Nyeupe ambamo aliweza kuthibitisha ya kwamba galaksi yetu inazunguka kwenye mhimili wake.

Alionyesha kitovu cha Njia Nyeupe kina umbali wa takriban miakanuru 30,000 kutoka Dunia akakadiria ya kwamba masi ya Njia Nyeupe inalingana na masi ya Jua mara bilioni 100.[4].

Alikuwa pia kati ya wataalamu wa kwanza waliotumia wimbiredio kwa kupima nyota.[5]

Oort alikadiria kuwepo kwa wingu la magimba madogo yanayozunguka mfumo wa Jua letu kwa umbali mkubwa sana ambalo ni asili ya nyotamkia zenye obiti ndefu[6]. Masi hii inaitwa Wingu la Oort. Halikuweza kuthibitishwa bado lakini linalingana na makadirio yote kuhusu mwendo wa nyotamkia.

Kuanzia mwaka 1958 hadi 1961 Oort alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (UKIA).

Marejeo

  1. Van De Hulst H.C. 1994. "Jan Hendrik Oort. 28 April 1900-5 November 1992". Biographical Memoirs of Fellows of the Royal Society. 40: 320–326. doi:10.1098/rsbm.1994.0042.{{cite journal}}: CS1 maint: numeric names: authors list (link)
  2. "Jan Hendrik Oort: Comet Pioneer". European Space Agency. Iliwekwa mnamo 30 Mei 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Wilford, John. "Jan H. Oort, Dutch astronomer in forefront of field, dies at 92", 12 November 1992. Retrieved on 30 May 2014. 
  4. Oort J.H. 1970. Galaxies and the universe: properties of the universe are revealed by the rotation of galaxies and their distribution in space. Science 170 (3965): 1363–1370. [1] Archived 17 Agosti 2017 at the Wayback Machine.
  5. Woltjer, Lodewijk 1993. "Obituary: Jan H. Oort". Physics Today. 46 (11): 104–105. Bibcode:1993PhT....46k.104W. doi:10.1063/1.2809110. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-10-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-22. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: numeric names: authors list (link)
  6. yaani zinazorudi baada ya miaka mingi

Viungo vya nje