Guruguru (nusufamilia)

(Elekezwa kutoka Gerrhosaurinae)
Guruguru
Guruguru koo-njano (Gerrhosaurus flavigularis)
Guruguru koo-njano (Gerrhosaurus flavigularis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Lacertilia (Mijusi)
Familia ya juu: Scincoidea (Mijusi kama mijusi-islam)
Familia: Gerrhosauridae
Nusufamilia: Gerrhosaurinae
Ngazi za chini

Jenasi 5, spishi 18:

Guruguru, kwa fasiri nyembamba, ni mijusi wa nusufamilia Gerrhosaurinae katika familia Gerrhosauridae. Spishi za nusufamilia nyingine, Zonosaurinae, zinaitwa guruguru-visiwa. Mijusi hawa wana magamba magumu mgongoni. Mbavuni wana kunyanzi la ngozi kwa urefu mzima wa mwili. Mkia wa spishi za jenasi Tetradactylus ni mrefu sana, zaidi ya mara mbili ya urefu wa mwili. Na miguu yao ni mifupi au haipo. Kwa sababu ya hiyo huitwa guruguru-nyoka.

Nusufamilia hii ina spishi kubwa kabisa za Afrika: hadi sm 75. Lakini spishi nyingi ni sm 30-45. Huishi kati ya mawe na miamba, katika vishimo, katika vichuguu au takataka ya majani na matawi. Chakula chao ni wadudu hasa, kama panzi, mchwa na sisimizi, lakini majongoo, tandu, konokono na mijusi wengine pia, na spishi nyingine hula matunda na maua pia.

Spishi

hariri

Marejeo

hariri
  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Guruguru (nusufamilia) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.