Ghulam Ali (mwimbaji)
'
Ghulam Ali khan
غلام علی خان ਗੁਲਾਮ ਅਲੀ ਖਾਨ ग़ुलाम अली ख़ान | |
---|---|
Ghulam Ali akiwa Chennai | |
Amezaliwa | 5 Desemba 1940 Kalekay Nagra, Punjab, British India (Pakistan ya sasa) |
Kazi yake | Mwimbaji |
Ustad Ghulam Ali (kwa Kiurdu: غُلام علی; amezaliwa 5 Desemba 1940) ni mwimbaji wa ghazal kutoka nchini Pakistan wa Patiala Gharana. Pia amekuwa mashuhuri kwa uchezaji. Ghulam Ali alikuwa mwanafunzi wa Bade Ghulam Ali Khan (elder Ghulam Ali Khan). Ali pia alifundishwa na kaka zake Bade Ghulam Ali - Barkat Ali Khan na Mubarak Ali Khan.
Ghulam Ali anachukuliwa kuwa mmoja wa waimbaji bora wa ghazal wa enzi yake. Mtindo wake na tofauti zake katika kuimba Ghazals zimetajwa kuwa za kipekee, kwani anachanganya muziki wa kitamaduni wa Hindustani na ule wa ghazal, tofauti na mwimbaji mwingine yeyote wa ghazal. Ghulan ni maarufu sana nchini Pakistan, India, Afghanistan, Nepal, Bangladeshi, na pia miongoni mwa watu wa Asia Kusini walioishi Amerika, Uingereza na nchi za Mashariki ya Kati.[1]
Ghazals zake nyingi maarufu zimetumika katika sinema za Bollywood. Ghazals zake maarufu ni pamoja na Chupke Chupke Raat Din, Kal Chaudhvin Ki Raat Thi, Hungama Hai Kyon Barpa, Chamakte Chand Ko, Kiya Hai Pyar Jis, Mei Nazar Sé Pee Raha Hoon, Mastana Peeyé, Yé dil yé pagal dil, Apni Dhun Mein Rehta Hoon ghazal na Nasir Kazmi, "Ham Ko Kiske Gham Ne Maara". Albamu yake ya hivi karibuni "Hasratein" iliteuliwa katika kitengo cha Albamu Bora ya Ghazal kwenye Tuzo za Star GIMA 2014. Alikuwa amemwooa Afsana Ali na wana binti aitwae Manjari Ghulam Ali.
Mnamo mwaka wa 2015, kwa sababu ya maandamano ya Shiv Sena huko Mumbai, tamasha lake lilifutwa.[2] Baadae, alipokea mialiko kutoka kwa Waziri Mkuu wa Delhi Arvind Kejriwal, Waziri Mkuu wa Bengal Magharibi Mamata Banerjee na Waziri Mkuu wa Uttar Pradesh Akhilesh Yadav.[3] Baada ya kughairiwa, alitumbuiza huko Lucknow, India,[3] New Delhi na huko Trivandrum, na Kozhikode, Kerala, India.[4]
Katika habari iliyoripotiwa mnamo 2015, Ghulam Ali alisema kwamba hatafanya maonyesho huko India siku zijazo. Alisema kuwa hataki kutumiwa kwa masuala ya kisiasa.[4]
Maisha ya awali
haririJina lake 'Ghulam Ali' alipewa na baba yake, shabiki mkubwa wa Bade Ghulam Ali Khan ambaye, zamani, alikuwa akiishi Lahore. Ghulam Ali alikuwa akimsikiliza Khan kila wakati tangu utoto wake.
Ghulam Ali alikutana na Ustad Bade Ghulam Ali Khan, kwa mara ya kwanza, wakati alikuwa katika ujana wake. Ustad Bade Ghulam Ali Khan alikuwa amezuru Kabul, Afghanistan na, wakati wa kurudi India, baba yake Ghulam Ali alimwomba Ustad amchukue mwanawe kama mwanafunzi. Lakini Khan alisisitiza kwamba kwa kuwa hakuwa karibu na mjini, mafunzo ya kawaida hayangewezekana. Lakini baada ya maombi ya mara kwa mara kutoka kwa baba ya Ghulam Ali, Ustad Bade Ghulam Ali Khan alimwuliza kijana Ghulam Ali kuimba kitu. Haikuwa rahisi kuwa na ujasiri wa kuimba mbele yake. Alijipa ujasiri wa kuimba Thumri "Saiyyan Bolo Tanik Mose Rahiyo Na Jaye." Baada ya kumaliza, Ustad alimkumbatia na kumfanya mwanafunzi wake.[1]
Kazi
haririGhulam Ali alianza kuimba ndani ya Redio Pakistan, Lahore mnamo 1960. Pamoja na kuimba ghazals, Ghulam Ali anatunga muziki kwa ghazals yake. Nyimbo zake ni za raga na wakati mwingine ni pamoja na mchanganyiko wa kisayansi wa ragas. Anajulikana kwa kuchanganya Gharana-gaayaki ndani ya ghazal na hii inaupa uimbaji wake uwezo wa kugusa mioyo ya watu. Anaimba nyimbo za Kipunjabi pia. Nyimbo zake nyingi za Kipunjabi zimekuwa maarufu na zimekuwa sehemu ya ugawanyiko wa kitamaduni wa Punjab. Ingawa katokea Pakistan, Ghulam Ali bado ni maarufu nchini India kama vile alivyo Pakistan. Asha Bhosle amefanya albamu za pamoja za muziki naye.
Alitambulishwa kwenye sinema ya Kihindi na wimbo wa filamu wa Kihindi Chupke Chupke Raat Din ulioandikwa na mshairi Hasrat Mohani katika filamu ya B. R. Chopra, Nikaah (1982).[5] Ghazals nyingine maarufu ni pamoja na Hungama Hai Kyon Barpa na Awaargi. Mara nyingi huchagua ghazal za washairi mashuhuri.
Wakati akiulizwa juu ya vikundi vya pop vya Pakistani, Ghulam Ali alijibu, "Kwa kweli, nimeshangazwa sana na mtindo wao wa kuimba. Je! Unawezaje kuimba wimbo kwa kukimbia, kururuka na kuzunguka jukwaani? Jukwaa linalenga kutumbuiza sio sarakasi."[1]
Ghulam Ali pia ameimba ghazals za Kinepali kama Kina kina timro tasveer, Gajalu tee thula thula aankha, Lolaaeka tee thula na Ke chha ra diun katika lugha ya Kinepali na Narayan Gopal, mwimbaji anayejulikana wa Nepali, na mtunzi Deepak Jangam. Nyimbo hizo ziliandikwa na Mfalme Mahendra wa Nepal. Nyimbo hizi zilikusanywa katika albamu inayoitwa Narayan Gopal, Ghulam Ali Ra Ma, na ni maarufu kati ya wapenzi wa muziki wa Kinepali hadi leo.[1]
Moja ya matamasha yake ya kukumbukwa ilikuwa katika Taj Mahal.[6] Alipoulizwa juu ya siku zijazo za waimbaji wa ghazal, alisema alifurahiya waimbaji maarufu kama mwimbaji wa ghazal Adithya Srinivasan, ambaye alifanya kazi ya ufunguzi kwenye tamasha lake mnamo 2012 huko Bangalore.[7] Hivi karibuni, mnamo Februari 2013, maestro alikua mtu wa kwanza kupokea tuzo ya Bade Ghulam Ali Khan. Akizungumzia hili, alisema, "Nina deni kwa serikali ya India kwa kunipa tuzo hii. Kwangu, ni tuzo kubwa zaidi ambayo nimepokea kwa sababu imepewa jina la guru langu." Alipata pia tuzo ya kwanza ya Swaralaya Global Legend (2016) huko Trivandrum, Kerala, India.[8] Ghulam Ali pia alikuwa mwimbaji wa chaguo la Marehemu Mfalme wa Nepal Mahendra Birbikram Shah Dev. Ghulam Ali aliimba nyimbo kadhaa maarufu zilizoandikwa na Mfalme Mahendra.[1]
Ghazals/ nyimbo mashuhuri
hariri- Aah ko chahiyye ek umr asar honey tak (mshairi: The Great Mirza Ghalib)[9]
- Ae husn-e-beparwah tujhe shola kahoon ya shabnam kahoon (mshairi: Bashir Badr)
- Apni Dhun Mein Rehta Hun, Mai Bhi Tere Jaisa Hun (mshairi: Nasir Kazmi)[10]
- Apni Tasveer Ko Aankhon Se (mshairi: Shahzad Ahmad)
- Arz-e-gham say bhi faaida tou nahin (mshairi: Raees Warsi)
- Awaargi (mshairi: Mohsin Naqvi)
- Teri Yaad Yaad (mshairi: Sameer)
- Saaqi Sharab Laa
- Baharon ko Chaman
- Barsan Lagi Sawan Bundiya Raja (mshairi: Traditional)
- Bata do tum humein bedaad karna (mshairi: Riaz Khairabadi)
- Bechain bahut phirna ghabraaye huye rehna (mshairi: Munir Niazi)
- Chamakte Chand Ko Tuta Hua Tara Bana Dala (mshairi: Anand Bakshi)
- Chhup Chhupa Ke Piyo
- Chupke Chupke Raat Din (mshairi: Hasrat Mohani)[5][1][9]
- Dard-e-dil dard aashna jaane (mshairi: Bahadur Shah Zafar)
- Dareeche Be-sada Koi Nahin Hai (mshairi: Sabir Zafar)
- Dil Buk Buk Ahro
- Dil Jala Ke Mera Muskuraate Hain Woh
- Dil dhadakne ka sabab yaad aaya (mshairi: Nasir Kazmi)
- Dil Mein Ek Leher Si Uthi Hai Abhi (mshairi: Nasir Kazmi)[6][9]
- Fasle Aise Bhi Honge (mshairi: Adeem Hashmi)
- Gajalu Ti Thula Thula Aankha (mshairi: King Mahendra of Nepal)[10]
- Hadaff-e-Gham na kiya sang-e-mallamat nay mujhay (mshairi: Raees Warsi)
- Heer (Punjabi Traditional)
- Hum Tere Shahar Mein Aaye Hain Musafir Ki Tarha
- Hum To Kitnon Ko Mahzabeen Kehte Hain
- Humko Kiske Gham Ne Mara (mshairi: Masroor Anwar)
- Hungama Hai Kyon Barpa (Akbar Allahabadi)[9][10]
- Itni muddat baad mile ho (mshairi: Mohsin Naqvi)
- Jin ke honton pe hansi
- Kachhi Deewar Hoon Thokar Na Lagana
- Kaisi Chali Hai Abke Hawa
- Kal Chaudhvin Ki Raat Thi (mshairi: Ibn-e-Insha)[9][10]
- Kal Raat Bazm mein jo mila
- Kehte Hain Mujhse Ishq Ka Afsana Chahiye (Qamar Jalalabadi)
- Khuli Jo Aankh (mshairi: Farhat Shehzad)[9]
- Khushboo Gunche Talash Karti Hai
- Khushboo Jaise Log Mile
- Ki Pucchde Ho Haal (Punjabi song)
- Kina Kina Timro Tasveer(Nepali Song)[10]
- Kiya Hai Pyaar Jise (mshairi: Qateel Shifai)[9][10]
- koi humnafas nahi hai
- koi ummid bar nahi aati (mshairi: Ghalib)[9]
- Lolayeka ti thula (Nepali Song)
- Main Nazar Se Pee Raha Hoon[10]
- Mehfil Mein Baar Baar (Agha Bismil)
- Mere shoq da nai aitbar tenu mshairi: Ghulam Mustafa Tabassum
- Niyat-e-shauq bhar na jaaye kahin (mshairi: Nasir Kazmi)
- Ni Chambe Diye Bandh Kaliye (Punjabi song)
- Nit de vichore sada (Punjabi song)
- Pata laga mainu huun ki judai (Punjabi song)
- Patta Patta Boota Boota (mshairi: Meer Taqi Meer)
- Paara Paara Hua Pairaahan-e-Jaan (mshairi: Syed Razid-e-Ramzi)
- Pehli waari aj hona (Punjabi song)
- Phir Kisi Rahguzar Par Shahyad (mshairi: Ahmed Faraz)
- Phir Sawan Rut Ki Pawan Chali, Tum Yaad Aaye (mshairi: Nasir Kazmi)
- Rabba Mere Haal Da (Punjabi song)
- "Rahe ishq ki inteha chahata hoon"
- Ranj Ki Jab Guftagu Hone Lagi (mshairi: Daag Dehlavi)
- Roya Karenge Aap Bhi (mshairi: Momin Khan Momin)[10]
- Shauq Har Rang Raqeeb-E-Sar-O-Samaan Nikla (mshairi: Ghalib)[9]
- Tak Patri Waaleya Lekh Mere (Punjabi song)
- Tamaam Umr Tera Intezar Kiya (mshairi: Hafeez Hoshiarpuri)
- Tumhare Khat Mein Naya Ik Salaam Kis Ka Thaa (mshairi: Daag Dehlavi)[10]
- Woh Kabhi Mil Jayen Tau (mshairi: Akhtar Sheerani)[10]
- Woh Jo Hum Mein Tum Mein Qarar Tha (mshairi: Momin Khan Momin)[10]
- Yeh Batein Jhooti Batein Hain mshairi: Ibn-e-Insha[10]
- Yeh Dil Yeh Pagal Dil (mshairi: Mohsin Naqvi)[10]
- Zakhm-e-Tanhai Mein Khusboo-e-Heena Kiski Thi
- Zehaal-e-miskin mukun taghaful (mshairi: Amir Khusroo)[9]
Diskografia
hariri- Tere Shehar Mein – 1996[10]
- Lamha Lamha – 1997
- Mahtab – 1997
- Madhosh – 1999
- Khushboo – 2000
- Rabba Yaar Milaade – 2000
- Passions – 2000
- Sajda – 2001
- Visaal – 2004[9]
- Aabshaar – 2006
- Parchhaiyan – 2006
- Husn-E-Ghazal – 2007
- The Enchanter – 2010
- Anjuman Behtareen Ghazalein[10]
- At His Very Best Ghulam Ali
- Aawargee
- Dillagee
- Ghazalain – Live at Islamabad[10]
- Ghazals
- Great Ghazals
- Geet Aur Ghazals
- Hungama Live in Concert Vol.1[10]
- Haseen Lamhe
- Khwahish
- Live in USA Vol 2 – Private Mehfil Series
- Live in USA Vol 1 – Private Mehfil Series
- Mast Nazren -Ecstatic Glances Live in London, 1984[10]
- Narayan Gopal, Ghulam Ali Ra Ma (Nepali Ghazals)[10]
- Once More
- Poems of Love
- Saadgi
- Suraag – In Concert
- Suno
- Soulful
- Saugaat
- The Golden Moments – Patta Patta Boota Boota
- The Finest Recordings of Ghulam Ali
- The Golden Collection
- With Love
- Kalaam-E-Mohabbat (Ghazals written by Sant Darshan Singh Ji)
- Chupke Chupke – Live in Concert, England
- Rang Tarang vol 1,2
- Janay Walay
- Heer
- Ghulam Ali – The Very Best
- Ghulam Ali – Mehfil – Collection From Live Concerts
- The Best of Ghulam Ali
- Awargi—Ghulam Ali – Vocal CDNF418/419 Live. Vol.3 & 4.
- Aitbaar
- Aadaab Ustad (Ghazals)
- Ghulam Ali Vol.1 and 2
- A Ghazal Treat – Ghulam Ali in Concert;;
- Ghulam Ali in Concert
- Awargi (Live) Vol 1 and 2
- Moods and Emotions
- Ek Ehsaas – A Confluence of the Finest Ghazal Voices
- Best of Ghulam Ali
- Greatest Hits Of Ghulam Ali
- The Golden Moments Ghulam Ali (Vol.1)[10]
- A Live Concert
- The Best of Ghulam Ali
- Once More[10]
- Mehraab
- Ghulam Ali Live at India Gate – Swar Utsav 2001 – Songs of the Wandering Soul[10]
- Ghalib – Ghazals – Ghulam Ali – Mehdi Hassan
- The Latest, the best"\
- Meraj-E-Ghazal, Ghulam Ali & Asha Bhosle[9][10]
Tuzo na kutambuliwa
haririMarejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Legendary singer Ghulam Ali — Part IV". apnaorg.com. Iliwekwa mnamo 2021-04-11.
- ↑ https://www.nytimes.com/2015/10/09/world/asia/pakistan-singer-ghulam-ali-concert-canceled-india.html
- ↑ 3.0 3.1 "Ghulam Ali Performs in Lucknow, Meets Akhilesh Yadav". NDTV.com. Iliwekwa mnamo 2021-04-11.
- ↑ 4.0 4.1 "Ghulam Ali doesn't want to be used for political mileage; won't perform in India". Zee News (kwa Kiingereza). 2015-11-04. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-11. Iliwekwa mnamo 2021-04-11.
- ↑ 5.0 5.1 "Ghulam Ali". IMDb. Iliwekwa mnamo 2021-04-11.
- ↑ 6.0 6.1 Nimisha Tiwari | TNN | Jul 10, 2007, 00:00 Ist. "Ghulam Ali sings in praise of the Taj | undefined News - Times of India". The Times of India (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-04-11.
{{cite web}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link) - ↑ "From the words of Ghalib ... | Deccan Chronicle". web.archive.org. 2013-12-03. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-12-03. Iliwekwa mnamo 2021-04-11.
- ↑ Reporter, Staff (2016-01-15), "Swaralaya award presented to Ghulam Ali", The Hindu (kwa Indian English), ISSN 0971-751X, iliwekwa mnamo 2021-04-11
- ↑ 9.00 9.01 9.02 9.03 9.04 9.05 9.06 9.07 9.08 9.09 9.10 9.11 To Ghulam Ali With Love Ilihifadhiwa 3 Machi 2016 kwenye Wayback Machine. Technofundo.com website, Published 19 September 2007. Retrieved 16 July 2019
- ↑ 10.00 10.01 10.02 10.03 10.04 10.05 10.06 10.07 10.08 10.09 10.10 10.11 10.12 10.13 10.14 10.15 10.16 10.17 10.18 10.19 10.20 10.21 10.22 10.23 Amjad Parvez (8 Aprili 2014). "Legendary singer Ghulam Ali". Academy of the Punjab in North America (APNA) website. Iliwekwa mnamo 16 Julai 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
hariri[[Jamii:Wanamuziki nchi kwa nchi|P]