Panya-vichaka

(Elekezwa kutoka Grammomys)
Panya-vichaka
Panya-vichaka wa nyika
Panya-vichaka wa nyika
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wanyama wagugunaji)
Nusuoda: Myomorpha (Wanyama kama panya)
Familia: Muridae (Wanyama walio na mnasaba na panya)
Nusufamilia: Murinae (Wanyama wanaofanana na panya)
Jenasi: Grammomys
Thomas, 1915
Ngazi za chini

Spishi 15:

Panya-vichaka ni wanyama wagugunaji wa jenasi Grammomys katika nusufamilia Murinae ya familia Muridae ambao wanatokea Afrika kusini kwa Sahara katika misitu na nyika nyevu ambapo wanaishi mitini.

Maelezo

hariri

Panya-vichaka wana manyoya mafupi na magumu. Mgongo ni aina ya kahawia au kijivu zaidi, upande wa chini ni mweupe. Wana mkia mrefu wenye manyoya membamba na masikio makubwa yenye umbo la duaradufu. Miguu ya nyuma ni myembamba kiasi na kidole cha tano ni kifupi. Urefu wa mwili ni mm 80-140, urefu wa mkia mm 120-220 mm na uzito ni g 28-65.

Panya hao wanaishi mitini katika misitu minyevu na maeneo mengine yenye miti na/au vichaka. Hula matunda, mbegu, mizizi na vyakula vingine vya mimea, kama gome, na pengine wadudu. Hukiakia usiku.

Viota vyao vina ukubwa wa sm 15-30 na vimo kwenye miti kwa urefu wa m 0.5-2. Mimba huchukua kama siku 24 na mikumbo ya hadi wachanga 4 hutolewa.

Spishi

hariri