Hallonflickan au "Binti wa Luttra" ni jina la mabaki ya maiti ya mwanamke aliyekufa takriban miaka 5000 iliyopita na ambaye mifupa yake ilihifadhiwa katika matope ya kinamasi.

Kiunzi cha mifupa cha Hallonflickan, Falbygdens museum.
Fuvu la kichwa la Hallonflickan.

Alipatikana katika eneo la kijiji cha Luttra kwenye kata ya Falköping, Uswidi, mwaka 1943. Uchunguzi wa kitaalamu uliweza kuthibitisha ya kwamba aliwahi kula matunda ya rasiberi, kwa hiyo alipewa jina la "binti wa rasiberi" (hallon-flickan) kwa lugha ya Kiswidi. Meno yanaonyesha ya kwamba alifikia umri wa miaka 18 - 25.