Hammurabi (takr. 1810 KK - 1750 KK) alikuwa mfalme wa sita wa mji wa Babeli akapanua eneo lake na kuunda milki ya kwanza ya Babeli. Anajulikana hasa kwa mkusanyo wa sheria za Hammurabi ambazo ni kati ya sheria za kwanza za dunia zilizoandikwa.

Sehemu ya juu ya nguzo ya Hammurabi yenye sheria zake yamwonyesha mfalme Hammurabi mbele ya mungu Marduk.
Babeli, 1792 - 1750 KK.

Hammurabi alirithi ufalme kutoka kwa baba yake akitawala eneo la mji wa Babeli kama dola-mji tu. Katika miaka ya utawala wake alifaulu kupanua himaya yake hadi kutawala Mesopotamia yote. Hivyo alianzisha milki ya kwanza ya Babeli.

Sheria za Hammurabi hariri

Umaarufu wake watokana na sheria zake. Hakuwa mtawala wa kwanza wa Mesopotamia aliyetunza sheria za milki kimaandishi. Lakini sheria nyingine zimepotea au kuhifadhiwa kwa sehemu tu. Mkusanyo wa sheria za Hammurabi ni wa kwanza uliosambazwa kiasi cha kuwa na nakala nyingi, hivyo nakala kadhaa zimehifadhiwa hadi leo na kutupa picha ya jamii ile ya kale sana.

Nakala maarufu ni nguzo ya jiwe kubwa lenye kimo cha mita 2.25 inayomwonyesha mfalme mbele ya mungu Marduk na chini yake ziko sheria katika mwandiko wa kikabari.

Sheria hizi zilikuwa kali sana. Mfano wake ni vipengele vifuatavyo:

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hammurabi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.