Hekalu la Artemis mjini Efeso

Hekalu la Artemis mjini Efeso (kwa Kigiriki ὁ ναὸς τῆς Ἀρτέμιδος Ἐφεσίης, τὸ Ἀρτεμίσιον (ho naòs tês Artémidos Ephesíês, tò Artemísion), kwa Kilatini: Templum Dianae Ephesi(n)ae au Artemisium Ephesi(n)um) lilikuwa jengo kubwa la kidini lililojulikana kote katika mazingira ya Mediteraneo wakati wa Ugiriki wa Kale na Roma ya Kale.

Maghofu ya hekalu huko Efeso

Hekalu hilo lilihesabiwa kati ya maajabu saba ya dunia.

Historia

hariri

Lilijengwa mjini Efeso kwa muda wa miaka 120 kuanzia mwaka 560 KK. Mfalme Kroisos wa Lidia ndiye aliyeanzisha ujenzi huu.

Hekalu lilikuwa na urefu wa mita 115 na upana wa mita 55. Nguzo zake zilisimama mita 18.

Liliharibika na kujengwa upya mara kadhaa. Mwaka 262 BK liliharibiwa kabisa wakati wa uvamizi wa Wagodoni.

Leo hii kuna nguzo moja tu inayoonekana.

  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hekalu la Artemis mjini Efeso kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.