Maajabu ya dunia

(Elekezwa kutoka Maajabu saba ya dunia)

Maajabu ya dunia ni orodha ya majengo saba ya pekee iliyojulikana na Wagiriki wa Kale. Wagiriki waliita majengo hayo ΤÀ ΕΠΤÀ ΘΕÁΜΑΤΑ ΤΗΣ ΟΙΚΟΥΜÉΝΗΣ (ΓΗΣ) ta hepta theamata tes oikumenes (ges) - Maajabu saba ya dunia inayokaliwa).

Maajabu saba ya dunia ya kale
Orodha ya makala yafuatana na picha hizi saba

Mara ya kwanza majengo ya ajabu yaliorodheshwa na mwandishi Herodoti mnamo 450 KK. Ilhali maandiko yake hayakuhifadhiwa, habari hii inatokana na waandishi wengine waliomrejea. Kulikuwa na orodha tofauti[1][2] lakini ile inayojulikana na kutajwa zaidi ni ile ya Antipater wa Sidon[3]

Ilhali orodha hii ilikusanywa na waandishi wa Ugiriki ya Kale kuna majengo tu yaliyojulikana katika ustaarabu huo. Kwa hiyo hakuna mifano kutoka Uhindi, China, Asia ya Mashariki, Amerika, Afrika kusini ya Sahara wala Ulaya ya Kaskazini.

Majengo ya orodha ya Antipater hayakudumu hadi leo, isipokuwa Piramidi za Giza. Mengine yaliharibika kutokana na matetemeko ya ardhi au kubomolewa, tena hadi leo hapajulikani mahali pa "Mabustani ya Semiramis". Sanamu na picha za kuchongwa kutoka Kaburi la Mausolo na Hekalu la Artemis zilikusanwa na kuhifadhiwa katika Makumbusho ya Britania mjini London, Uingereza.

Maajabu saba ya Kale Edit

  1. Piramidi za Giza (Misri ya Kale)
  2. Mabustani ya Semiramis (Babeli, leo Irak)
  3. Hekalu ya Artemis mjini Efeso ((Ugiriki ya Kale, leo Uturuki, Asia Ndogo)
  4. Sanamu ya Zeus mjini Olympia (Ugiriki ya Kale)
  5. Kaburi la Mausolo mjini Halikarnassos (Ugiriki ya Kale, leo Uturuki)
  6. Sanamu ya Kolossos kisiwani Rhodos (Ugiriki ya Kale)
  7. Mnara wa Pharos ya Aleksandria (Misri)

Kati yake piramidi pekee zimebaki hadi leo.

Maajabu ya dunia ya sasa Edit

Katika ulimwengu kila siku maajabu yanaongezeka na kufanya maajabu mapya ya dunia kukubalika mara kwa mara. Kwa mfano, mwaka 2016 kuna maajabu yake. Orodha ya maajabu hayo hutolewa na watu mbalimbali kwa mitazamo tofautitofauti: wengine wanaishia upande wa majengo, wengine wanahesabu hata mazuri ya uasilia n.k.

Vitu hivi hadi kufikia kuitwa maajabu ya dunia ina maana ni vya pekee duniani kote, na hakuna kitu kingine kama hicho au cha kufanana nacho.

Tanzania kuna kitu kimoja ambacho kinasemekana ni kati ya maajabu ya dunia ambacho ni kasoko ya Ngorongoro, iliyoko mkoa wa Manyara.

Picha za "Maajabu ya Kisasa" Edit

Tazama pia Edit

Tanbihi Edit

  1. History of the Past: World History.
  2. Paul Lunde (May–June 1980). The Seven Wonders. Saudi Aramco World. Iliwekwa mnamo 2009-09-12.
  3. Antipater, Greek Anthology IX.58

Marejeo Edit

Viungo vya nje Edit

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maajabu ya dunia kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.