Helier Mtakatifu
Helier Mtakatifu (alifariki 555) alikuwa mkaapweke anaheshimika kama mmisionari wa kisiwa cha Jersey, karibu na Ufaransa[1].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana tarehe 16 Julai[2].
Maisha
haririMtoto wa wazazi tajiri wa Tongeren (leo nchini Ubelgiji). Ingawa Wapagani walikubali mtoto alelewe Kikristo, ila walipomuua Kunibert, mlezi wake, Helier alitoroka nyumbani.
Hatimaye alifikia Cotentin alipojiunga na monasteri ya Marcouf huko Nantus (Nanteuil, sasa St.-Marcouf-de-l’Isle, Manche).
Ni Marcouf aliyempeleka pamoja na padri Romard kuinjilisha Jersey ambapo hatimaye aliuawa na maharamia kwa kukatwa kichwa[3].
Tazama pia
haririTanbihi
haririVyanzo
hariri- A Biographical Dictionary of Jersey, G.R. Balleine
- A Theory on the Evangelisation of the Cotentin (Normany Peninsular):St Marculf, M. Charles Grosset
- Elizabeth Castle by Major NVL Rybot
Viungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
- Article on St Helier by G.R. Balleine Ilihifadhiwa 25 Machi 2008 kwenye Wayback Machine.
- "St. Elier or Helier, Hermit and Martyr", Butler's Lives of the Saints
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |