Kiguudau

Ndege wa maji wa familia Heliornithidae
(Elekezwa kutoka Heliornithidae)
Kiguudau
Kiguudau wa Afrika
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Gruiformes (Ndege kama korongo)
Familia: Heliornithidae (Ndege walio na mnasaba na viguudau)
G.R. Gray, 1840
Ngazi za chini

Jenasi 3, spishi 3:

Viguudau ni ndege wa maji wa familia Heliornithidae. Familia hii ina spishi tatu tu, kila moja katika jenasi yake. Ndege hawa wana mwili mwembamba, shingo ndefu, mkia mpana na domo lenye ncha kali. Wana tando za ngozi kati ya vidole vyao zinazowasaidia kuogelea. Wanatokea kanda za tropiki kwa maji yatiririkayo polepole au katika vinamasi na mabwawa ya mikoko. Hula wadudu, makoa, gegereka, vyura na samaki wadogo. Hujenga tago lao la vitawi na mimea kwa matete.

Spishi ya Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri