Herma wa Roma alikuwa kati ya Wakristo wa kwanza wa jiji la Roma, Italia, katika karne ya 1.

Mtume Paulo katika Waraka kwa Warumi alimtumia salamu zake (Rom 16:14).

Inasemekana alipata kuwa askofu wa Filipopoli, leo Plovdiv, nchini Bulgaria.

Pengine anachanganywa pia na Herma, mwandishi wa kitabu cha karne ya 2 "Mchungaji" kama walivyofanya Origen, Eusebi wa Kaisarea na Jeromu[1].

Tangu kale anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali ya Ukristo kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 9 Mei[2], 8 Machi au 4 Novemba.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Herma wa Roma kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.