Hifadhi ya Kitaifa ya Wood Buffalo
Hifadhi ya Kitaifa ya Wood Buffalo ni mbuga ya kitaifa nchini Kanada iliyo mbuga ya kitaifa kubwa zaidi nchini. Hifadhi hiyo iko kaskazini mashariki mwa jimbo la Alberta na maeneo ya kusini ya Northwest Territories.
Iliteuliwa na UNESCO kama eneo la Urithi wa Dunia mnamo 1983 kwa sababu ya bioanuwai inayopatikana hapo. Ndani yake iko delta ya Peace-Athabasca ambayo inahesabiwa kati ya delta kubwa zaidi ya maji matamu duniani. Kuna idadi kubwa ya ng'ombe mwitu aina ya baisani, pamoja na spishi mbalimbali za wanyama wa pori.
Tovuti za Nje
hariri- Wood Buffalo National Park; Parks Canada
- Wood Buffalo National Park; UNESCO