Bioanuwai

kiwango cha tofauti ya aina za maisha

Bioanwai (pia baioanwai; kwa Kiing. biodiversity) ni dhana ya biolojia inayoleenga kueleza wingi wa anwai za spishi za kibiolojia katika mazingira fulani, pamoja na wingi wa jeni katika mimea na wanyama wa eneo fulani.

Ramani ya kanda za bioanwai duniani; kanda za tropiki huwa na idadi kubwa ya spishi tofauti

Umuhimu wa bioanwai

hariri

Bioanwai ni muhimu kwa sababu viumbehai wote wanategemeana kwa namna fulani.

  • Misitu ni makazi ya wanyama
  • Wanyama hula mimea
  • Mimea hutegemea udongo wenye tabia fulani kwa ustawi wake
  • Fungi zinasaidia kuozesha mimea na wanyama waliokufa
  • Wadudu kama nyuki hubeba chavua kutoka mmea mmoja hadi mwingine na hivyo kuwezesha mimea mingi kuzaa
  • Kama bioanwai hiyo katika makazi fulani inapungua, uhusiano baina ya pande zake unafifia na pande zote zinaweza kupata hasara.

Bioanwai ni muhimu kwa binadamu kwa namna nyingi. Mimea hutoa oksijeni na kusafisha hewa chafu. Mimea hutoa pia chakula, kivuli, vifaa vya ujenzi, dawa na nyuzi za nguo na karatasi. Mizizi ya mimea inapunguza mmomonyoko na mafuriko. Mimea, fungi na wadudu hutunza rutuba ya udongo na kusafisha maji. Kadri bioanwai inavyopungua, mifumo hiyo inaharibika.

Mfano ni matumizi ya kemikali katika kilimo yaliyolenga wadudu wanaoharibu mazao; lakini dawa hizo zunaathiri wadudu wote; katika nchi zenye matumizi makubwa ya dawa hizo idadi ya wadudu kwa jumla imepungua na kuhatarisha kustawi kwa mimea mingi pamoja na kilimo cha matunda.

Kuelewa na kutunza bioanwai ni shabaha muhimu katika hifadhi ya mazingira.

Viungo vya Nje

hariri
 
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Taarifa

hariri

Marejeo

hariri