Hifadhi ya bahari ya Dar es Salaam

Hifadhi ya bahari ya Dar es Salaam inajumlisha maeneo kadhaa kwenye Bahari Hindi karibu na Dar es Salaam, Tanzania. Kwa jumla kuna visiwa tisa visivyokaliwa na watu pamoja na sehemu za bahari kati ya visiwa hivi. Kuna visiwa vinne upande wa kusini wa Dar es Salaam ambavyo ni Bongoyo, Mbudya, Pangavini na Fungu Yasini, halafu vitano upande wa kusini ambavyo ni (Makatumbe, Finda na Kenda). Hifadhi hii inalinda sehemu za matumbawe, za miti ya mikoko na mimea mingine chini ya uso wa maji.

Hifadhi ya bahari ya Dar es Salaam
Dar es Salaam Marine Reserve System

Fungu Yasini reef
Nearest cityDar es Salaam
Eneo15 km²
Mamlaka ya utawalaMarine Parks & Reserves Authority (Tanzania)
Tovuti rasmi

Utawala hariri

Utawala wa hifadhi ya bahari umo mikononi mwa bodi ya wadhamini wa Hifadhi na Maeneo Tengefu ya Bahari.

Maeneo tengefu ya bahari ya Dar es Salaam yalianzishwa kufuatana na sheria ya uvuvi ya mwaka 1970 [1] yakipelekwa baadaye kwa idara ya Hifadhi na Maeneo Tengefu ya Bahari [1] Archived 29 Septemba 2007 at the Wayback Machine..

Matumizi na matatizo hariri

Visiwa vya Bongoyo na Mbudya hasa vinatembelewa mara nyingi na watalii wageni na wazalendo pia wanaofika kwa kuogelea, kupumzika ufukoni, kutazama matumbawe au kutembea visiwani. Hata hivyo idadi kubwa ya wageni wasiosimamiwa imesababisha matatizo ndani ya maeneo tengefu.

Wavuvi wa Kunduchi, Unonio, na Msasani wanategemea samaki waliopo katika maeneo tengefu. Mashindano kati ya wavuvi pamoja na uhaba wa usimamizi yalisababisha uharibifu hasa kwa kutumia nyavu za kukamata samaki zilizo ndogo na pia mabomu yanaoharibu matumbawe pamoja na samaki changa.

Viungo vya nje hariri

 
Pangavini Island
  1. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-05-15. Iliwekwa mnamo 2017-01-23.