Hudihudi

Ndege wa familia Upupidae wenye ushungi mrefu
Hudihudi
Hudihudi wa Ulaya
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Bucerotiformes (Ndege kama hondohondo)
Familia: Upupidae (Ndege walio na mnasaba na hudihudi)
Jenasi: Upupa
Linnaeus, 1758
Ngazi za chini

Spishi 4:

Hudihudi au ndututu ni ndege wa familia Upupidae wenye ushungi mrefu na domo refu na jembamba. Hudihudi wa Afrika huitwa jogoo-mwitu au kwembe kisunzu pia. Mwili una rangi ya machungwa lakini mabawa ni meusi yenye miraba myeupe na mkia pia ni mweusi na una mraba mweupe mmoja. Ndege hawa wanatokea maeneo wazi wa Afrika, Asia na Ulaya. Hutafuta chakula chini wakipenya ardhi kwa domo lao, pengine hukamata wadudu hewani. Hula wadudu hasa lakini watambaachi na vyura wadogo, mbegu na beri pia. Tago lao ni tundu mtini, katika ukuta wa nje au mwamba au ndani ya kando ya mchanga. Jike huyataga mayai 6-10.

Spishi

hariri