Hudihudi
Ndege wa familia Upupidae wenye ushungi mrefu
(Elekezwa kutoka Upupidae)
Hudihudi | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 4:
|
Hudihudi au ndututu ni ndege wa familia Upupidae wenye ushungi mrefu na domo refu na jembamba. Hudihudi wa Afrika huitwa jogoo-mwitu au kwembe kisunzu pia. Mwili una rangi ya machungwa lakini mabawa ni meusi yenye miraba myeupe na mkia pia ni mweusi na una mraba mweupe mmoja. Ndege hawa wanatokea maeneo wazi wa Afrika, Asia na Ulaya. Hutafuta chakula chini wakipenya ardhi kwa domo lao, pengine hukamata wadudu hewani. Hula wadudu hasa lakini watambaachi na vyura wadogo, mbegu na beri pia. Tago lao ni tundu mtini, katika ukuta wa nje au mwamba au ndani ya kando ya mchanga. Jike huyataga mayai 6-10.
Spishi
hariri- Upupa africana, Hudihudi wa Afrika (African Hoopoe)
- Upupa antaios, Hudihudi Mkubwa (Giant au Saint Helena Hoopoe) imekwisha sasa (karne ya 16)
- Upupa epops, Hudihudi wa Ulaya (Eurasian Hoopoe)
- Upupa marginata, Hudihudi wa Madagaska (Madagascar Hoopoe)
Picha
hariri-
Hudihudi wa Afrika
-
Hudihudi wa Madagaska
-
Mayai ya hudihudi wa Ulaya